1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Udanganyifu wa Uchaguzi hadi kwenye Ushindi

3 Novemba 2009

Duru ya pili ya uchaguzi wa rais uliyopangwa kufanyika nchini Afghanistan Jumamosi ijayo umefutwa.Rais wa hivi sasa Hamid Karzai hatimae ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa Agosti 20 alioufanyia udanganyifu.

https://p.dw.com/p/KMes
Afghan President Hamid Karzai gestures to journalists as he heads to receive U.N. Secretary-General Ban Ki-moon, unseen, at the presidential palace in Kabul, Afghanistan, Monday, Nov. 2, 2009. Afghanistan's election commission has canceled Saturday's presidential runoff and proclaimed Karzai victor of the war-ravaged nation's tumultuous ballot. (AP Photo/Ahmad Masood, Pool)
Rais wa Afghanistan Hamid Karzai.Picha: AP

Uamuzi uliopitishwa na tume, iliyo huru kwa jina tu, ni kilele cha kiinimacho cha uchaguzi kilichoendelea zaidi ya miezi miwili iliyopita. Tume hiyo kwa kweli, ni Halmshauri ya Uchaguzi iliyo na wafuasi wa Karzai. Bila ya shaka, umma wa Afghanistan umepoteza imani yake kwa wote waliohusika - kuanzia wanasiasa wa Afghanistan, Marekani na washirika wake wa Magharibi na hata Umoja wa Mataifa na huenda ikawa shida sana kuirejesha tena imani hiyo.Kwa hivyo, tangu kuanzishwa kwa operesheni ya kimataifa nchini Afghanistan hapo mwaka 2001,chini ya uongozi wa Marekani kuleta utulivu katika nchi iliyoteketezwa kwa vita,ugaidi na rushwa,sasa kuna uwezekano mdogo sana kwa operesheni hiyo kufanikiwa.

Hata uamuzi wa kuiweka serikali kuu mjini Kabul kwa matumaini ya kuleta amani na udhibiti kwanza katika mji huo mkuu na baadae kote nchini, ulikuwa wa mashaka. Kwani kihistoria, Afghanistan kamwe haikuwa na serikali kuu iliyoweza kweli kuidhibiti nchi nzima. Daima ni wakuu wa kikabila na viongozi wa kivita waliokuwa na mamlaka mitaani na majimboni. Hata ikiwa miaka minane iliyopita halikuwepo chaguo jingine ila kuunda serikali kuu,baadae kulifanywa makosa mengine pia.

Karzai anaetokea kabila kubwa la Pashtu, aliteuliwa kuwa rais bila ya kushauriana vya kutosha pamoja na makundi mengine madogo ya kikabila nchini humo. Hadi hii leo, rais huyo hajafanikiwa kuudhibiti kikamilifu mji mkuu Kabul. Vile vile nchi za magharibi zimemstahmilia kwa muda mrefu Karzai anaesita kuchukua hatua kali dhidi ya rushwa na biashara ya madawa ya kulevya na hata yeye binafsi akituhumiwa. Licha ya sauti kupazwa hata nchini Marekani kumlaumu Karzai, nchi za Magharibi ziliendelea kumuunga mkono.

Nchi hizo vile vile zilificha kuwa wakati wa kampeni za uchaguzi,Karzai alisikilizana na wakubwa wa vita na wafanyabiashara wa madawa ya kulevya na kuwaahidi kuwa akishinda, atawapatia nyadhifa serikalini na jeshini. Hata udanganyifu mkubwa uliofanywa wakati wa uchaguzi wa Agosti 20 ulifichwa. Serikali ya Marekani na washirika wake wengine wa NATO nchini Afghanistan, tangu mwanzo wa mwezi wa Oktoba walitaka kumtangaza Karzai mshindi wa uchaguzi huo.

Afghan President Hamid Karzai, left, talks with U.N. Secretary-General Ban Ki-moon at the presidential palace in Kabul, Afghanistan, Monday, Nov. 2, 2009. The U.N. chief made a surprise visit to Afghanistan on Monday as Afghanistan's election commission has canceled Saturday's presidential runoff and proclaimed Karzai victor of the war-ravaged nation's tumultuous ballot. (AP Photo,Reuters/Ahmad Masood, Pool)
Rais Karzai na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.Picha: AP

Hata Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alitoa ridhaa yake na naibu kiongozi wa umoja huo nchini Afghanistan aliachishwa kazi kwa sababu alitaka pafanyike uchunguzi wa madai ya kufanyika udanganyifu, wakati wa uchaguzi.Kwa hivyo, inaeleweka mpinzani wa Karzai, Abdullah Abdullah alipopinga kushiriki katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais.

Mwandishi:A.Zumach/ZPR

Mhariri:M-Abdul-Rahman