1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Udondozi wa magazeti

Sekione Kitojo26 Agosti 2010

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wameangalia zaidi leo kuhusu suala la ulinzi wa data za wafanyakazi, kusitishwa sheria ya kuwaandikisha vijana jeshini kwa mujibu wa sheria na Westerwelle.

https://p.dw.com/p/OwvA
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle (FDP) akikutana na waziri mkuu wa Bulgaria Boyko Borissov.Picha: picture alliance/dpa

Tunafungua  sasa  kurasa  za  magazeti  ya  Ujerumani ambapo  wahariri  wa  leo  wametuwama  zaidi  katika suala  la  ulinzi  wa  data  za  wafanyakazi, kusitishwa  kwa sheria  ya  kuwaandikisha   vijana   kutumikia  jeshi   kwa mujibu  wa  sheria  na  pia  madai  ya  kutaka  waziri  wa mambo  ya  kigeni  wa  Ujerumani , Guido  Westerwelle kujiuzulu.

Tukianza na  gazeti   la  Frankfurter  Rundschau, linaandika  kuhusu  ulinzi  wa  data  za  wafanyakazi, katika mahali  pa  kazi.

Gazeti  linaandika  kuwa  muswada  wa  sheria  hiyo  pia hauko  timilifu , ili  kuweza  kushughulikia  suala  la kuwalinda  wafanyakazi  dhidi  ya  waajiri  wao  ambao  ni wadadisi. Hii  inahusiana  na  kupigwa  marufuku  uwekaji wa  kamera  katika  maeneo  ya  kazi. Waajiri  wanalipinga suala  hilo  la  kupigwa  marufuku, kwa  msingi  kuwa linazuwia  kuwadhibiti  wale  wafanyakazi  ambao  ni wadokozi.

Gazeti  la  Abendzeitung  la  mjini  Munich , kuhusiana  na mada  hiyo  linaandika.

Kwa  wafanyakazi  wa  kuajiriwa  wanaweza  kuwa  katika hali  ya kudhalilishwa, anasema  makamu  wa   mkuu  wa kundi  la  wabunge  wa   vyama  vya  CDU  na  CSU  katika bunge  la  Ujerumani , Michael  Fuchs. Haiwezekani , kwamba  wafanyakazi  wanacheza  tu  katika  mtandao  wa internet  kutwa  nzima. Hapa  anashauri  Fuchs haiwezekani  mfanyakazi  kuwa  amepata  mafunzo, na wakati  huo  huo akawa  hana  ujuzi  wa  kutosha. Kwa  hali yoyote  iwayo  muajiri  ni  lazima  amlinde  dhidi  ya uhalifu.

Nalo  gazeti  la  Westfälische  Nachrichten  öa  mjini Münster , linazungumzia  mada  hiyo  hiyo.

Serikali  ya  Ujerumani  ni  wazi  imelazimishwa   kuingia katika  mjadala  huu. Baada  ya  kashfa  ya  ulinzi  wa  data katika  makampuni  ya  kuuza  biadhaa  ya  Lidl, kampuni la  simu , Telecom  na  shirika  la  reli , Deutsche  Bahn, serikali  hatimaye  imeweza  kutoa  rasimu  ya  sheria, na kuweka  mipaka  ya  uchunguzi  wa  wafanyakazi. Sheria hiyo  ambayo  imeidhinishwa  tayari  na  baraza  la mawaziri, anaiangalia  mhariri  kuwa  ni  ya  dunia asiyoifahamu. Anasema  mhariri, kwa  hiyo  si  muhimu basi  kupiga  marufuku  uchukuaji  wa  data  kutoka  katika mitandao  ya  kijamii  katika  internet?

Mada  nyingine  iliyoandikwa   na  wahariri  wa  magazeti ya  Ujerumani  , inahusu  kusitishwa  kwa  sheria  ya kuwaandikisha  vijana   jeshini  kwa  mujibu  wa  sheria. Gazeti  la  die tagespost la  mjini  Würzburg  linaandika.

Ikiwa  jeshi  la  Ujerumani  Bundeswehr likiundwa   hivi karibuni   na  wanajeshi  wa  kuajiriwa  na  wale  wa  muda, au  wa  kujitolea  basi  hilo  litakuwa  jeshi  la  kampuni  ya ulinzi. Iwapo  jeshi  hilo  litapoteza  uhusiano  na  jamii  ya Ujerumani , kwa  kuwafanya  watu  wa  taifa  hili kutotumikia  jeshi  hilo  kwa  mujibu  wa  sheria, basi itavunja moja  kati  ya  mhimili  mkuu  ambao  pia  uko katika  katiba  ya  nchi  hii. Na iwapo  jengo  hilo  litavunjika, basi  itakuwa  imeundwa  nafasi  mpya  ya  matamanio yasiyoweza  kudhibitiwa  ya  uzalendo  na  hali  ya kutovumilia hali  ambayo  jamii  yetu  haihitaji.

Gazeti  la  der  neue tag  linaandika  kuhusu  madai  ya kutaka  waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Ujerumani ajiuzulu. Gazeti  linaandika.

Paka  akitoka  panya  hutawala. Guido Westerwelle anafahamu  hilo. Lakini  pamoja  na  kufahamu  hilo, wakati wote Westerwelle  amekuwa  akijishughulisha   tu  na mambo  ya  kigeni. Kwa  hiyo  wakati  akiwa   katika  ziara yake  hivi  sasa   ya  mataifa  ya  eneo  la  Balkan , huku nyuma  kuna  wito  unaotolewa  kutaka  ajiuzulu. Viongozi wenzake  wanashindwa  kumkingia  kifua. Shutuma  za Rainer  Brüderle  kutokana  na  matokeo  mabaya  ya uchaguzi  uliopita  ni  hatari  kwake. Kutokana  na uchunguzi  wa  maoni  ya  wapiga  kura   kuwa  chini , anapaswa  kufanyia  kazi  hilo  ili  kubadili  hali  hiyo  katika chama  chake.

Mwandishi : Sekione  Kitojo / Inlandspresse

Mhariri : Mwadzaya,Thelma