1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Udugu wa Kiislamu wabanwa zaidi

26 Septemba 2013

Serikali ya Misri imeyafunga makao makuu ya gazeti "Uhuru na Haki" ambalo linalomilikiwa na chama cha Udugu wa Kiislamu ikiwa ni hatua ya mwanzo yenye lengo la kuvurga kabisa harakati za chama hicho.

https://p.dw.com/p/19oFI
epa03880893 (FILE) A file photo dated 01 July 2013 shows an Egyptian opposing President Mohamed Morsi waving Egyptian flag after storming the headquarters of the ruling Muslim Brotherhood, at al-Moqattam suburban, Cairo, Egypt. A court in Cairo on 23 September banned the Muslim Brotherhood of ousted president Mohamed Morsi and ordered the confiscation of its assets. The ruling specifically banned "all activities by the group, and any affiliated institutions." The court recommended that the cabinet forms an independent committee to follow up on the implementation of the ruling. EPA/KHALED ELFIQI +++(c) dpa - Bildfunk+++
Jengo lililoshambuliwa la chama cha udugu wa Kiislamu mjini CairoPicha: picture-alliance/dpa

Katika taarifa yake iliyotolewa leo (25.09.2013) katika mtandoa wa facebook, chama cha Udugu wa Kiislamu kimesema "Sisi waandishi habari wa gazeti la Uhuru na Haki tunalaani kitendo cha vikosi vya usalama kufunga makao makuu ya gazeti".

Usiku wa kuamkia leo, jeshi la polisi lilizishambulia ofisi hizo na kuondoa nyaraka kadhaa zilizokuwemo. Chanzo kimoja kutoka katika kitengo cha usalama cha Misri kimesema hatua hiyo inatokana na uamuzi wa mahakama wa Jumatatu, wa kupiga marufuku chama hicho na kuamuru kudhibitiwa hazina yake.

Vurugu ni sababu za operesheni

Akiendeleza kutoa ufafanuzi kuhusu namna wanavyoendesha operesheni hiyo chanzo hicho kimesema uamuzi wa mahakama ambao umesababasha kutekelezwa kwa hatua hiyo kunatokana na kuwepo kwa mashitaka ya kuchochea vurugu pamoja na vitendo vya ugaidi kulikoteka katika siku za hivi karibuni.

An Egyptian supporter of the Muslim Brotherhood walks holding a poster featuring deposed president Mohamed Morsi during a rally to support him on July 6, 2013 outside Cairo's Rabaa al-Adawiya mosque. Egypt's Islamists vowed further protests today to demand the army restore the country's first democratically elected leader, after a day of clashes which saw 26 people killed across the country. AFP PHOTO/MAHMUD HAMS (Photo credit should read MAHMUD HAMS/AFP/Getty Images)
Mfuasi wa chama cha Udugu wa KiislamuPicha: Mahmud Hams/AFP/Getty Images

Mwezi Julai mwaka huu, jeshi lilimuondoa madarakani rais Mohamed Mursi ambapo pia chama chama chake cha Udugu wa Kiislamu kimeshuhudia mikasa ya mamia ya wanachama wake kuuwawa na wengine maelfu kukamatwa tangu wakati huo.

Waandishi 50 wawakwepa polisi

Kampeni hii ya sasa ya vikosi vya usalama imelazimisha vilevile zaidi ya waandishi habari 50, ambao wanafanikisha uchapishaji wa kila siku wa gazeti hilo "Uhuru na Haki" kufanya kazi kwa kujificha kwa lengo la kukwepa kutiwa mbaroni.

Jina la gazeti hilo limetolewa na tawi moja la kisiasa la chama cha Udugu wa Kiislamu kikiwa na shabaha ya kufanya harakati za kumrejesha madarakani Mohamed Mursi, baada ya mapinduzi ya kijeshi dhidi ya kiongozi huyo aliyechaguliwa kidemokrasia.

Chama cha Udugu wa Kiislamu kiliibuka kutoka gizani na kushinda katika chaguzi na bunge na rais baada ya kuondolewa madarakani kiongozi wa kiimla Hosni Mubarak kufuatia vuguvugu la mwaka 2011 nchini humo.

Idadi kubwa ya Wamisri waligawanyika baada ya Mohamed Mursi kujilimbikizia madaraka na kushindwa kuukwamua uchumi na kuwafanya waingie mitaani kumpinga, jambo ambalo pia lilisababisha jeshi kuingilia kati. Wengi wa raia hao kwa hivi sasa wanamtukuza kiongozi wa kijeshi Jenerali Abdel Fattah al-Sisi kutokana na hatua ya kufanikishwa kuondolewa madarakani Mohamed Mursi.

Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Josephat Charo