1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uefa Euro 2012 : sasa ni robo fainali

21 Juni 2012

Wachezaji, maafisa na mashabiki wamepata mapumziko mafupi katika fainali za ubingwa wa Ulaya,Jumatano ,(20.06.2012), lakini manung'uniko ya Ukraine ambayo ni mwenyeji mwenza wa mashindano haya yanaendelea.

https://p.dw.com/p/15In8
epa03270613 Portuguese national soccer team fans celebrate in downtown Porto after the 2-1 against the Netherlands and being qualified for the quarterfinals at the end of Group B preliminary round match of the UEFA EURO 2012, 17 June 2012, Portugal. EPA/ESTELA SILVA
Mashabiki wa UrenoPicha: picture alliance/dpa

Ukraine wamejiunga  na  wenyeji  wenza  Poland  kuwa  ni  pumba   katika mashindano  haya   baada  ya  kushindwa  kwa  bao  1-0  dhidi  ya Uingereza  na  gumzo  lilituwama  katika  goli  ambalo  halikuwa, ambalo  refa  aliamua  kuwa  halikuvuka  mstari  lililofungwa  na wenyeji  hao  dhidi  ya  Uingereza.

Haki haikutendeka

Hisia  za  kutotendewa  haki  nchini  Ukraine  hazikuweza  kupozwa na  Pierluigi Collina, mkuu  wa  waamuzi  katika  shirikisho  la kandanda  barani  Ulaya  Uefa, kwa  kukiri  kuwa  goli  lile  lilipaswa kukubaliwa.

Italian referee Pierluigi Collina arrives for the Euro 2004 Group B soccer match between England and Croatia at the Luz Stadium in Lisbon, Portugal, Monday June 21, 2004. The other teams in Group B are Switzerland and France. (AP Photo/Adam Butler)
Mkuu wa marefa wa Uefa Pierluigi CollinaPicha: AP

Ukraine  pia  bado  inaendelea  kupambana  na  maandamano kuhusiana  na  kufungwa  kwa  waziri  mkuu  wa  zamani  Yulia Tymoshenko , wakati  serikali  ya  Uingereza  ikisema  itasusia pambano  la  robo  fainali  kati  ya  Uingereza  na  Italia  mjini  Kiev siku  ya  Jumapili  kwa  kutomtuma   waziri  wake  huko.

Kansela uwanjani

Kansela  wa  Ujerumani Angela  Merkel  ambaye  ni  shabiki  mkubwa wa  timu  ya  taifa , hakuhudhuria  michezo  yote  mitatu  ya  makundi nchini  Ukraine  lakini  atahudhuria  mchezo  wa  robo  fainali   dhidi ya  Ugiriki  katika  mji  wa  Gdanski  nchini  Poland   Ijumaa.

Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) und der mexikanische Präsident Felipe Calderon treffen am Montag (18.06.2012) in Los Cabos, Mexiko, zusammen. Am 18. und 19.06.2012 findet in dem exklusiven Badeort am Pazifik der diesjährige G20-Gipfel statt. Foto: Peer Grimm dpa
Kansela MerkelPicha: picture-alliance/dpa

Wachezaji  na  makocha  kutoka  Ujerumani  na Ugiriki  wameamua kutotoa  umuhimu  wa  pekee  katika  mchezo  huo  ambao umegeuza  hisia  katika  mashindano  hayo  kuelekea  katika  mzozo wa  kiuchumi  unaoathiri  mataifa  kadha  yanayohusika.

Vyombo  vya  habari  vya  Ugiriki  hata  hivyo  vinashauku  ya  nafasi hii  ya  kuirejesha  timu  ya  Ujerumani  nyumbani  mbele  ya  kiongozi wa  taifa  hilo, ambaye  hapendwi  nchini  Ugiriki kutokana  na  hatua kali  za  kubana  matumizi  ambazo  ameilazimisha  nchi  hiyo kuchukua , ili  kuweza  kupata  mkopo  wa  kimataifa wa  kuiokoa kiuchumi.

Refa  kutoka  Hungary  Viktor Kassai  na  msaidizi  wake  katika mstari  wa  goli  hawapendwi  kabisa  na  mashabiki  wa  Ukraine baada  ya  kutokubali  goli  lililowekwa  wavuni  na  Marco Devic, ambalo  halingeweza  kuwaweka  wenyeji  hao  wenza  katika  robo fainali  lakini lingefanya  hali  kuwa  mbaya  kwa  Uingereza.

Wakati  mashindano  haya  yamebakisha  timu  nane   na  taji linaonekana   ghafla  mbele  ya  timu  hizi  baada  ya  michuano  ya kufurahisha  ya  makundi, mtanange  unaanza  tena  upya  leo Alhamis (21.06.2012)  wakati  robo  fainali  zitakapoanza   mjini Warsaw  kati  ya  Jamhuri  ya  Czech  itakapokwaana  na  Ureno.

Nani atapeta

Nahodha  wa  Czech  Tomas Rosicky  ana matumaini  kuwa  fiti  kwa mchezo  huo  baada  ya  kupata  maumivu  ya  misuli.

Ujerumani  inamiadi  na  Ugiriki mjini  Gdanski   Ijumaa, (22.06.2012), wakati  mabingwa  watetezi  Uhispania  inakipiga  na Ufaransa  mjini  Donetsk  siku  ya  Jumamosi  na  Uingereza itakamilisha  ratiba  hii  ya  michuano  ya  robo  fainali  siku  ya Jumapili  kwa  kutiana  kifuani  na  Italia  mjini  Kiev.

Greece's Kostas Chalkias (C) talks to his team mates during their Group A Euro 2012 soccer match against Czech Republic at the city stadium in Wroclaw, June 12, 2012. REUTERS/Dominic Ebenbichler (POLAND - Tags: SPORT SOCCER)
Kikosi cha Ugiriki, wazee wa kulinda langoPicha: Reuters

Wakati  huo  huo  Croatia  imekabiliwa  na  madai  ya  pili  ya ubaguzi  siku  ya  Jumatano  kuhusiana  na  mabango  yaliyowekwa wakati  waliposhindwa  kwa  bao  1-0  dhidi  ya  Uhispania  na kuyaaga  mashindano  haya.

Croatia  tayari  imekwisha  pigwa  faini  ya  euro  80,000  baada  ya mashabiki  kuelekeza  matusi  ya  kibaguzi  dhidi  ya  mshambuliaji wa  Italia  Mario Balotelli  na  kufyatua fashifashi  katika  mpambano wa  Croatia  katika  kundi  la  pili  mjini  Poznan. Pia  wamepigwa faini  ya  euro  25,000  kwa  matukio kati  ya  mashabiki  katika mchezo  wao  wa  ufunguzi.

Mwandishi : Sekione  Kitojo / rtre