1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UEFA Kumekucha

9 Juni 2012

Fainali za kombe la mataifa ya Ulaya,EUFA-EURO 2012, ambayo safari hii yanaandaliwa kwa ubia na Poland na Ukraine yanaanza saa chache kutoka sasa. Pambano la ufunguzi ni kati ya Poland na Ugiriki.

https://p.dw.com/p/15Azt
Mashabiki wa kabumbu
Mashabiki wa kabumbuPicha: picture-alliance/dpa

Mashabiki wa soka wa Poland wakivalia nguo zenye rangi ya bendra yao ya taiafa , nyeupe na nyekundu, walianza kumiminika mapema leo mchana kuungana na mashabiki kutoka sehemu nyengine za Ulaya kuujaza uwanja wa watazamaji 100,000 mjini Warsaw, tayari kwa sherehe za ufunguli pamoja na pambano hilo la kwanza .

Wengi wameelezea matumaini na timu yao, hasa kutokana na kuwa na wachezaji kadhaa katika ligi za Ulaya . Lakini kwa upande mwengine kandoni mwa matarajio ya ushindi kuna kiwewe.

Mashabiki wa kabumbu
Mashabiki wa kabumbuPicha: AP

Kocha wa Poland Franciszek Smuda ameungama kwamba alisahau hata kusherehekea tarehe ya harusi yake kwa sababu ya mashindano haya aya Euro 2012. Hata mkewe Malgorzata alikiri kwamba naye pia alisahau kwamba ni mwaka wa tano wa harusi yao, kwa sababu ya kombe hili la mataifa ya Ulaya .

Baba Mtakatifu hayuko kando na michezo hiyo

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Benedikti XVI inaelekea naye hatojiweka kando na mashindano haya . Leo alitowa wito akiomba yawe ya amani na furaha akisema mashindano hayo sio tu yanawaleta pamoja waandalizi, wachezaji na mashabiki wa kandanda bali pia jamii kwa jumla.

Mjini Wroclaw ambako usiku wa leo Urusi itamenyana na Jamhuri ya Cheki, tayari wapenzi wa kandanda wakirusi wapatao 10,000 wa Wacheki 6,800 walikuwa wakisubiri kuwa miongoni mwa watazamaji 40,000 uwanjani.

Katika jiji la Kiev mji mkuu wa Ukraine lilifunguliwa a eneo maalum la mashabiki wa mashindano hayo kwa muziki ngoma za asili , vifijo na nderemo.

Mashabiki wakiwa na bendera za taifa lao
Mashabiki wakiwa na bendera za taifa laoPicha: DW

Nchini Ujerumani wapenzi pamoja na kuweko kawa shauku ya kuanza kwa mashindano haya ya kombe la mataifa ya Ulaya , mwapenzi wa kabumbu awanalisubiri pia pambano la kesho kati ya Ujerumani na Ureno.

Mshambuliaji mkongwe wa kikosi cha Ujerumani Miroslav Klose ambaye atakuwa pia akisherehekea miaka 34 ya kuzaliwa , anasema zawadi muwafaka anayoitarajia kesho ni ushindi na kuondoka na pointi tatu dhidi ya Ureno.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman/DPA/AFP

Mhariri: Saumu Mwasimba