1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufalme wa miaka 240 wa Nepal sasa watoweka

24 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cfjv

KATMANDU:

Serikali ya Nepal imepiga kura kuufutilia mbali ufalme katika nchi hiyo.Viongozi wa Nepal wakubaliana mpango ambao utawajumulisha tena waasi wa zamani wa kundi linalojiita la Mao, katika serikali na hivyo kuweka njia bayana ya kukomesha ufalme wa miaka 240. Wapaiganaji wa Mao walijiondoa kutoka serikali mwezi Septemba. Miongoni mwa madai muhimu ya waMao kujiunga tena na serikali ni kutangazwa kwa serikali hiyo kuwa Jamhuri.Hatua hiyo itatekelezwa mda si mrefu katika katiba ya mda ya nchi hiyo.Ufalme utabaki kama ulivyo hadi pale uchaguzi utakapofanywa mwaka ujao.