1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yalaani mauwaji ya Toulouse na Montauban

Oumilkher Hamidou20 Machi 2012

Msako dhidi ya muuwaji wa watu 4 katika shule 1 ya wayahudi mjini Toulouse .Hatua za usalama zimeimarishwa katika shule zote za kiyahudi,masinagogi na misikiti nchini Ufaransa.

https://p.dw.com/p/14Nk8
Shambulio dhidi ya shule ya kiyahudi mjini ToulousePicha: AP

Kwa mujbiu wa duru za karibu na wizara ya mambo ya ndani,wachunguzi wasiopungua 300 wametawanywa kila pembe kujaribu kumsaka na kumkamata bwana huyo aliyewauwa pia wanajeshi wanne,watatu wenye asili ya Afrika kaskazini-au Maghreb na mwengine wa kutoka Antilles, wiki iliyopita huko huko Toulouse na katika mji mwengine wa kusini Montauban.

"Mbali na wachunguzi hao,askari polisi wote wa Toulouse wameingia mbioni." Duru za wizara ya mambo ya ndani z inazungumzia juu ya askari kanzu elfu moja zaidi wanaomsaka muuwaji huyo.

Tangu asubuhi polisi wameanza kuingia katika nyumba za karibu na shule hiyo ya kiyahudi Ozar Hatorah,kaskazini mashariki ya mji wa Toulouse ili kukusanya ushahidi wa wale ambao pengine watakuwa wamemuona au kupitana na muuwaji huyo.

Frankreich Anschlag Schule Toulouse Sarkozy
Rais Sarkozy (kati kati) akihutubia jamii ya wayahudi katika shule ya Ozar HatorahPicha: AP

Mauwaji hayo yanayotisha yamelaaniwa na wagombea wote wa kiti cha urais nchini Ufaransa.Rais Nicolas Sarkozy na mpinzani wake mkubwa,Francois Hollande walifika Toulouse kuwapa pole waliopoteza walio wao.Rais Nicolas Sarkozy amekitaja kisa hicho "kuwa msiba mkubwa kuwahi kutokea na kuahidi" kitajibiwa kama inavyostahiki.Njia zote,tena njia zote zilizoko zitatumiwa ili kumzuwia mhalifu huyo asimdhuru mtu yeyote mwengine.""

Kamepni za uchaguzi zimesitishwa kwa siku moja na Ufaransa nzima ilikaa kimya kwa dakika moja,saa tano mchana kuomboleza na kulaani mauwaji hayo.

Juhudi za kumsaka mtuhumiwa huyo zinaendelea.Katika mahojiano pamoja na kituo cha televisheni cha Europe 1,waziri wa mambo ya ndani Claude Guéant amesema "kanda ya video imenasa baadhi ya maelezo kumhusu mtu huyo aliyekuwa akiendesha pikipiki wakati wa mauwaji hayo.

Claude Guéant aliyewasili Toulouse tangu jana usiku amedhibitisha ripoti za waandishi habari kwamba bwana huyo anaesakwa alikuwa na kamera ndogo ili kunasa yote aliyokuwa anayafanya.

Inasemekana hakuacha alama yoyote inayoweza kumfanya agunduliwe.

Frankreich Anschlag Schule Toulouse
Bwana huyo anajaribu kuwatuliza wanafunzi baada ya shambulioPicha: AP

"Ni habithi mkubwa hata kupata moyo wa kurikodi ukatili aliokuwa akifanya" amesema waziri wa mambo ya ndani Claude Guéant.

Akiulizwa kuhusu uwezekano wa shambulio la kigaidi,waziri wa mambo ya ndani amesema haijabainika kama muuwaji huyo ni mwanachama wa kundi lolote lile.

"Mjini Montauban,sawa na Toulouse,kote huko ameuwa akiwa peke yake.Suala linalozuka ni kama ana kundi la watu wanaomuunga mkono.Hilo hatujui bado.Lakini unapouwa watoto katika shule ya kiyahudi,hapo moja kwa moja kuna hisia za chuki dhidi ya wayahudi na hisia za ubaguzi."Amemaliza kusema waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Claude Guéant.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters/AFP

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman