1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufisadi duniani bado upo juu

9 Julai 2013

Watu wengi duniani wanaamini kuwa ufisadi umezidi huku mmoja kati ya watu wanne akikiri kutoa rushwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

https://p.dw.com/p/194dd
Nembo ya shirika la Transparency International
Nembo ya shirika la Transparency International

Shirika la kupambana na ufisadi duniani Transparency International limetoa ripoti leo inayoonyesha kuwa viwango vya ufisadi duniani bado viko juu lakini watu wana uwezo wa kuukomesha.Kati ya nchi kumi zilizotajwa,nane zinatokea barani Afrika.Na katika kanda ya Afrika mashariki Kenya bado inajikokota kukabiliana na ufisadi . Caro Robi amezungumza na afisa wa utafiti wa shirika hilo la Transparency nchini Kenya Bw Mwangi Kibathi na kwanza alimuuliza ni sekta gani zinazotajwa kuhusika pakubwa na tatizo hili? Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Caro Robi

Mhariri: Mohamed Abdulrahman