1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufunguzi wa Kituo maalum cha DW, jijini Dar es Salaam.

24 Februari 2010

Shirikal la Utangazaji la Kimataifa la Ujerumani DW, leo jijini Dar es Salaam, litaendesha mdahalo, kuhusu mchango wa vyombo vya habari kuelekea katika uchaguzi mkuu nchini Tanzania utakaofanyika baadaye mwaka huu.

https://p.dw.com/p/M9sa
Mhariri Mkuu wa DW, Marc Koch.Picha: Archiv

Lakini kabla ya mdahalo huo kufanya hivi sasa shughuli za ufunguzi rasmi wa kituo maalum cha kupata maelezo kuhusu matangazo ya DW zinaendelea katika mafunzo ya lugha ya Kijerumani ya Goethe jijini Dar es Salaam, Mbali na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, ufunguzi huo pia unahudhuriwa na Mhariri Mkuu wa DW, Marc Koch, Mkuu wa Idara ya matangazo ya Lugha za Afrika na mashariki ya kati wa DW Ute Schaeffer na Mkuu wa Idhaa ya Kswahili ya DW, Andrea Schmidt , wakishiriki pia wahariri mbalimbali wa vyombo vya habari nchini Tanzania pamoja na wageni wengine waalikwa.

Mwandishi: Halima Nyanza

Mhariri: Mohamed Abdulrahman