1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda: Viongozi wa kundi la M23 huenda wakafikishwa ICC

4 Aprili 2014

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje ,wa Uganda Henry Okello Oryem, amesema huenda baadhi ya viongozi wa waasi wa M23, wakafikishwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu dhidi ya binaadamu.

https://p.dw.com/p/1Bc5t
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Uganda Henry Okello Oryem
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Uganda Henry Okello OryemPicha: Getty Images/Afp/Phil Moore

Grace Kabogo amezungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Uganda, Ali Mutasa, ambapo kwanza alitaka kujua iwapo hatua hiyo inatokana na shinikizo lolote kutoka nje, hasa ikizingatiwa kuwa waasi wa M23 walikimbilia Uganda kwa usalama wao, nchi ambayo imekuwa ikidaiwa kuwasaidia waasi hao.

Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Grace Patricia Kabogo

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman