Uganda yangojea matokeo ya uchaguzi
19 Februari 2011Matangazo
Kiasi ya watu milioni 14 walikuwa na haki ya kupiga kura.Lakini kampeni ya uchaguzi iliingia dosari kufuatia madai kuwa chama tawala kilinunua kura. Sasa zoezi la kuhesabu kura zilizopigwa linaendelea huku Rais Museveni na mpinzani wake mkuu Kizza Besigye wa chama cha IPC, wakitabiri kuwa watashinda.Matokeo ya uchaguzi yanatazamiwa kutangazwa siku ya Jumapili.