1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ugiriki, Romania na Bulgaria wataka mazungumzo zaidi juu ya Kosovo.

23 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CfKQ

Brussels.

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Ugiriki , Romania na Bulgaria wametoa wito wa kuendeleza mazungumzo zaidi juu ya hali ya baadaye ya jimbo linalotaka kujitenga la Kosovo.

Mawaziri hao watatu ambao wamekutana mjini Athens siku ya Jumamosi wamesisitiza pia kuwa hali ya baadaye ya Serbia imo ndani ya umoja wa Ulaya na kuingia kwake katika umoja huo hakupaswi kufungamanishwa na hali ya mambo ya Kosovo. Majadiliano kuhusu Kosovo yalivunjika mapema mwezi huu baada ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kushindwa kufikia makubaliano. Nchi nyingi za umoja wa Ulaya pamoja na Marekani zinaunga mkono uhuru wa jimbo la Kosovo. Russia inaunga mkono msimamo wa Serbia kuwa jimbo hilo libaki chini ya himaya ya Serbia.