1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ugiriki yaidhinisha hatua za kubana matumizi

13 Februari 2012

Bunge la Ugiriki limeidhinisha hatua kali za kupunguza matumizi ya serikali katika juhudi ya kudhibiti uchumi wake unaoelekea kuporomoka.

https://p.dw.com/p/142O6
epa03102471 Greek Communist party MP Giorgos Mavrikos throws a booklet containing the new bailout deal for Greece during a parliament session in Athens, Greece, on 12 February 2012. Greece's parliament is to decide on whether to approve the new round of austerity measures that will allow the country facing bankruptcy to qualify for a second international bailout. EPA/PANTELIS SAITAS
Griechenland Parlament Abstimmung SparpaketPicha: picture-alliance/dpa

Mpango huo wa kubana matumizi unanuiwa kuipa nafasi kubwa Ugiriki kupokea mkopo wa euro bilioni 130 kuokoa uchumi wake kutoka kwa Umoja wa Ulaya na shirika la kimataifa la fedha duniani. Licha ya waandamanaji kuchoma jengo moja la Cinema, maduka na hata mabenki huku na kupambana vikali na vikosi vya kukabiliana na ghasia, kupinga mpango huo wa matumizi, bado wabunge walipiga kura na kupitisha mpango huo.

Kulingana na spika wa bunge Philippos Petsalnikos kati ya wabunge 278, ni 199 waliopiga kura ya ndio na wengine 74 kupinga mpango huo. Hata hivyo serikali hiyo ya muungano imewasimamisha kazi mara moja wabunge 43 wa vyama viwili vya waziri mkuu wa Ugiriki Lucan Papademos waliokwenda kinyume na mpango huo kutoka chama cha kisoshalisti cha PASOK na kile cha mrengo wa kulia cha New Democracy.

Mpango wa kubana matumizi uliopitishwa na bunge hilo usiku wa kuamkia leo unajumuisha kupunguza mishahara ya wafanyakazi kwa asilimia 22 na pia kupunguzwa kwa malipo ya uzeeni jambo ambalo limewakasirisha sana waandamanaji.

Ghasia zazuka

Kulingana na televisheni ya kitaifa nchini humo, ghasia kwa sasa zimesambaa hadi katika maeneo yanayotembelewa sana na watalii katika visiwa vya Corfu na Crete mjini Thessaloniki katikati mwa Ugiriki. Polisi wamesema takriban maduka 150 yalivamiwa na kuibwa huku majengo mengine 34 yakiteketezwa na waandamanaji hao.

Anti-austerity protesters draped with Greek flags stand in front of police guarding the parliament in Athens February 11, 2012 during a demonstration on the second day of a 48-hour strike by Greek workers unions. The Greek government told rebellious lawmakers on Saturday to back a deeply unpopular EU/IMF rescue in parliament or send the nation down "an unknown, dangerous path" to default and international economic isolation. REUTERS/Yannis Behrakis (GREECE - Tags: BUSINESS POLITICS CIVIL UNREST)//eingestellt von sti
Polisi wakikabiliana na waandamanajiPicha: Reuters

Wazima moto walikuwa na wakati mgumu kuuzima moto huo kutokana na idadi kubwa ya waandamanaji wanaokadiriwa kufikia 80,000 waliomiminika uwanjani katika maeneo ya bunge wakirusha mabomu ya petroli katika majengo mengine na kuwarushia mawe polisi wa kukabiliana na ghasia.

Kwa upande wake wizara ya afya imeripoti watu 54 kujeruhiwa. Waziri mkuu Lucas Papademos amelaani ghasia hizo na kusema kamwe ghasia hzitakubalika katika nchi hiyo ilio na demokrasia.

Evangelos Venizelos Waziri wa fedha wa Ugiriki amesema wizara yake haikuwa na budi ila kuunga mkono mpango huo, kwa kuwa iwapo serikali haitopokea mkopo kutoka Umoja wa Ulaya nchi hiyo itaporomoka vibaya kiuchumi.

Baada ya bunge la Ugiriki wa kuunga mkono hatua zaidi za kubana matumizi thamani ya sarafu ya euro ilipanda katika masoko ya hisa ya Asia na leo asubuhi .

Mwandishi Amina Abubakar/AFPE/RTRE

Mhariri Mohammed Abdul Rahman