1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ugiriki yenye madeni yapata pigo jipya

20 Septemba 2011

Serikali ya Ugiriki inayokabiliwa na kitisho cha kufilisika, imepata pigo jipya.

https://p.dw.com/p/Rmhv
Greek Minister of Finance Evagelos Venizelos speaks during a conference in Athens, Monday, Sept. 19, 2011. Greece's finance minister promised Monday to stick with his plan for the country to post a primary surplus in 2012, hours before he was to hold an emergency teleconference with debt inspectors. (Foto:Petros Giannakouris/AP/dapd)
Waziri wa Fedha wa Ugiriki, Evangelos VenizelosPicha: dapd

Mkutano uliofanywa jana usiku kwa njia ya simu pamoja na Umoja wa Ulaya, Benki Kuu ya Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, ulimalizika bila ya mafanikio makubwa.

Hata hivyo, Waziri wa Fedha wa Ugiriki, Evangelos Venizelos amesema, mazungumzo hayo yalikuwa na manufaa na umuhimu. Lakini bado kuna kazi kadhaa za kutekelezwa. Kwa mujibu wa Umoja wa Ulaya, leo jioni pia kutafanywa mkutano mwingine kwa njia ya simu.

Wakati huo huo, vyombo vya habari vinasema, serikali ya Ugiriki imepewa orodha ya hatua 15 zinazopaswa kutekelezwa haraka ili kubana matumizi. Ripoti ya wafadhili ndio itakayosaidia uamuzi kupitishwa, iwapo Ugiriki ipewe Euro bilioni 8 kutoka mfuko wa Euro bilioni 110. Habari rasmi zinasema, Ugriki inahitaji fedha hizo kwa dharura, ama sivyo itashindwa kukidhi gharama zake katika mwezi wa Oktoba.

World Bank President Robert Zoellick speaks during a press conference at World Bank's office in Beijing, China, Monday, Sept. 5, 2011. Zoellick said China can help boost tepid global economic growth by pressing ahead with reforms to promote its own domestic consumption. (Foto:Alexander F. Yuan/AP/dapd)
Rais wa Benki ya Dunia, Robert ZoelleckPicha: dapd

Wakati huo huo, Rais wa Benki ya Dunia, Robert Zoelleck ameonya kuwa mzozo wa madeni wa nchi tajiri zilizoendelea kiviwanda, vile vile unaathiri nchi zinazoinukia kiuchumi na zinazoendelea. Zoelleck, amesema, tayari kuna dalili za mwanzo katika masoko ya hisa na fedha. Akizungumza kabla ya kufunguliwa mkutano wa mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, mjini Washington, Zoelleck amesema, hivi sasa nchi zinazoinukia hazina uwezo wa kujikinga dhidi ya mzozo mpya wa kiuchumi. Ametoa mwito kwa nchi tajiri kuushughulikia kwa pamoja mzozo wao wa madeni.

Mada kuu katika mkutano huo wa mwaka, ni madeni makubwa ya baadhi ya nchi za Ulaya na hatari ya ukuaji wa kiuchumi kupungua kote duniani