1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhaba wa Mafuta nchini Tanzania

11 Agosti 2011

Nchini Tanzania bado uhaba wa mafuta unashuhudiwa jijini Dar es salaam,baada ya vituo vingi vya uuzaji bidhaa hiyo kuendelea kufungwa na vingine vikifungua lakini havina mafuta ya kuuza.

https://p.dw.com/p/12Ewc
Uhaba wa mafuta nchini TanzaniaPicha: picture-alliance/dpa

Hatua hii inajitokeza baada ya serikali kutoa agizo wiki hii kuwataka wauzaji wa bidhaa hiyo wafungue vituo vyao au wafutiwe leseni.Misururu ya magari bado inasemekana kuonekana katika vituo vichache vilivyofunguliwa.Aidha hali sio ya kawaida katika vituo hivyo kama alivyotueleza mmoja wa wamiliki wa vituo kadhaa vya mafuta katika jiji la Dar es salaam .

Mwandishi: Saumu Mwasimba

Mhariri:AbdulRahman