1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhamiaji haramu- Safari ya mauti

27 Aprili 2015

Kwa juma zima hili tunakuletea mfululizo wa habari, mahojiano na makala juu ya jaala ya maelfu ya watu wanaohatarisha maisha yao kuvuuka Bahari ya Meditterrenean kukimbilia Ulaya.

https://p.dw.com/p/1FFTt
04.2015 Flucht nach Europa Teaser

Bahari ya Mediterrenean inayoiunganisha Afrika ya Kaskazini na Ulaya imebadilishwa jina sasa na kuitwa "Bahari ya Mauti" kwani takribani kila siku mamia ya wahamiaji haramu kutoka Afrika na Asia hujaribu kuivuuka bahari hiyo katika jitihada zao wa kuingia barani Ulaya, wanakosema kuwa wanafuatia maisha mazuri. Matokeo yake wengi wao huzama wakiwa mkondoni, kwani wanatumia usafiri usio wa uhakika na wa kimagendo. Idadi ya vifo inazidi kupanda kila uchao.

Kwenye mtiririko huu wa makala, habari na mahijiano, Deutsche Welle inakuletea undani wa safari hizi, maisha ya kabla na baada ya safari kwa wale wanaofanikiwa kuvuuka, sababu halisi za wahamiaji haramu na juhudi zinazochukuliwa na dunia kukomesha safari hizi za mauti. Ungana nasi kila siku mchana kujifunza ukweli halisi.