1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uharibifu wa mazingira huenda ukaongezeka Brazil

18 Agosti 2017

Nchini Brazil, Wanamazingira wanamtuhumu rais wa Brazil kwa kushinikiza sheria itakayowanufaisha wafanyibiashara wa magogo na wapokonyaji ardhi katika eneo la msitu wa Amazon.

https://p.dw.com/p/2iRLK
Brasilien Kampf gegen illegale Abholzung
Picha: Reuters/U. Marcelino

Rais Michel Temer wa Brazil anaitegemea kamati yenye nguvu ya kilimo katika bunge la nchi hiyo katika kushinikiza pendekezo la mswada unaonuwia kupunguza maeneo ya uhifadhi ya msitu wa taifa wa Jamanxim katika jimbo la Para kwa asilimia 27 au karibu hektea 350,000 eneo lenye ukubwa karibu sana na Ureno.

Ikiwa mswada huo utapita, vizuizi juu ya kilimo na uchimbaji madini vitaondolewa katika maeneo yanayohifadhiwa, na wale waliokalia maeneo hayo kinyume na sheria  huenda wakapatiwa hati za umiliki ardhi.

Kulingana na mswada huo, maeneo tu yaliokaliwa kinyume cha sheria kabla msitu wa Jamanxim kufanywa kuwa mbuga ya wanyama mwaka 2006 yatahalalishwa.

Taasisi ya kitaifa ya Brazil inayohusika na utafiti kutoka angani ilibaini ukataji miti wa Amazon uliongezeka kwa asilimia 29 kuanzia Agosti 2015 hadi Julai 2016 baada ya kupungua pakubwa tangia mwaka 2015.

Mabadiliko ya sheria za ardhi nchini Brazil ya mwaka 2012 ambapo ahueni ilitolewa kwa wale walioshiriki katika njia zisizo halali za uharibifu wa misitu imeonekana kuwa ndio chanzo cha ongezeko huo wa uharibifu wa misitu na sababu hii imefanya taifa la Norway kama mwekezaji mkuu katika maswala ya kulinda misitu ikate msaada wake wa kifedha katika shughuli za kulinda msitu wa Amazon.

Brasilien Kampf gegen illegale Abholzung
Eneo ambalo limekatwa miti kinyume cha sheria, BrazilPicha: Reuters/U. Marcelino

Utunzaji Mazingira

Wataalamu wa maswala ya misitu wanasema kwamba uharibifu wa misitu hiyo unafanywa kwa kiwango kikubwa na wahalifu waliojipanga na wenye fedha ambao wanajishughulisha na kuiba ardhi ya umma na kuitumia kwa kuwekea mifugo yao , ukulima wa soya au uchimbaji madini na wahalifu hao mara nyingi wanakuwa na uhusiano wa karibu na uhussiano wa mitaa. wahalifu hao huwalipa wafanyakayi masikini kima kidogo cha fedha kwa ajili ya kukata miti ambayo baadaye wanaiuza kwa faida kubwa.

Mnamo mwezi wa Juni rais Tever alitia saini mabadiliko ya sheria ambayo wakosoaji wanasema mabadiliko hayo yanatoa msamaha kwa vitendo vya unyangànnyi wa ardhi kwasababu sheria hiyo imetoa msamaha kwa wale wote waliokali kinyume cha sheria ardhi ya umma kabla yamwaka 2011.

Mshirika mmoja wa karibu wa Rais Temer, Seneta Romero Juca ambaye ndiye pia mdhamini wa sheria hiyo anasema ni ya kihistoria. Alizungumzia pia deni lililolipwa kwa mamilioni ya familia waliohamia katika msitu wa Amazon katika miaka ya sabini na thamanini na ambao hawakukapata stakabadhi za kumiliki ardhi.

Hata hivyo walinzi wamazingira wanamlaumu rais Temer kwa kuutumia mswada wa kulinda misitu na hatua nyenginezo kwa kujiongezea umaarufu kutoka kwa makundi ya wafanyabiashara ya kilimo. Kundi hilo lina viti 230 kwenye bunge la Brazil. Hayo ni kwa mujibu wa shirika la kuteteta haki za Congressoem foco.

Mwandishi: Sam Cowie/DW São Paulo

Tafsiri: Fathiya Omar

Mhariri: Mohammed Khelef