1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhariri wa magazeti ya Ujerumani

16 Januari 2007

Harakati za waziri mkuu wa jimbo la Bavaria Edmund Stoiber akiwania uhai wake kisiasa na sera za rais George Bush wa Marekani katika mashariki ya kati ndizo mada zilizowashughulisha wahariri wa magazeti ya Ujerumani siku ya leo Jumanne. Udondozi wa magazeti ya Ujerumani leo hii mnaletewa na Sekione Kitojo.

https://p.dw.com/p/CHTx

Gazeti la Nordbayerische Kurier kutoka Bayreuth linazungumzia mzozo wa kisiasa katika chama cha CSU:

Linaandika:

Tetemeko la kisiasa linalotokea hivi sasa katika eneo la Bayern , linakichafua binafsi chama cha CSU, na waziri wake mkuu amedhurika kwa kiasi kikubwa. Usiku wa jana imeonekana dhahiri kuwa chombo cha CSU kinakwenda mrama. Nahodha wake anapaswa kuendelea kutoa mwelekeo, licha ya kuwa sehemu ya kikosi chake kimeasi.

Kwa kutoa chambo anaweza mtu kujaribu, kupata kuweza kuituliza hali ya mambo. Lakini ni ukweli usiokanika kuwa mwisho wa enzi ya Stoiber umefikia.

Gazeti la Stuttgarter Nachrichten nalo linaafiki kwa kusema.

Inaonyesha kwa sasa kuwa sio jambo tena ambalo haliwezekani, kuwa muda wa utawala wa Stoiber umebakiza muda huu tu wa majira ya baridi katika jimbo hilo. Lakini nyuma yake kuna manung’uniko yanayosikika zaidi na zaidi, kuwa waziri huyu mkuu hajafunga nia yake ya kutaka kugombea katika uchaguzi ujao wa chama. Anapenda Stoiber kupata ushindi katika mkwaruzano kama huu mara nyingine, lakini tayari amekwisha shindwa katika mpambano huu.

Mhariri wa gazeti la Ostthüringer Zeitung kutoka Gera anaadika:

Kile ambacho kinatokea huko Munich , hakieleweki. Kuna hali ya kumaliza kiongozi, wakati viongozi wa juu wakinyamaza kimya, kitu ambacho wanachama wa CSU hawatawasamehe. Hii inampa Stoiber kila wakati alama nyingi, kutokana na uwezo wake wa kupambana , nani kati ya wengine ambao wana mioyo dhaifu wangeweza hivi sasa kukiongoza chama hiki cha CSU pamoja na jimbo la Bayern.

Ni muda gain basi mchezo huu wa kuigiza utaendelea, zaidi ya hayo chama kinajiharibia pamoja pia na mtu atakayefuata katika uongozi.

Mhariri wa gazeti la Berliner Tagesspiegel anakitazama chama ndugu cha CDU katika taratibu zake.

Mhariri anaandika:

Kuna uwezekano kwamba wakiwa mbali na mji kunakotokea mchezo huo wa kuigiza, na wakiwa wanashughulika na shughuli zao mjini Bremen, viongozi wa CDU watakuwa wanajitafuna ulimi. Hakuna maelezo kutokana na mada hii, kutokana na lile linalotokea huko kila mmoja anajitafuna, kabla ya hapo kulikuwa na maneno ya kutuliza ya mwenyekiti , akisema Edmund Stoiber ni mtu mwenye kuheshimiwa, ambaye amekuwa akifanyakazi vizuri na chama cha CDU.

Chama cha CDU kinafahamu kuwa , kama ikitokea hali isiyoeleweka kwa CSU, pia nafasi ya chama cha CDU itakuwa mashakani. Na msingi wa madaraka ya Angela Merkel utakuwa mashakani.

Mhariri wa gazeti la Märkische Oderzeitung kutoka Frankfurt/Oder amejishughulisha zaidi na siasa za mashariki ya kati za utawala wa Marekani.

Mhariri anandika:

Miaka miwili imebaki kwa rais Bush kuwapo madarakani, katika awamu yake ya pili ya utawala hataki kuacha maafa katika sera za mambo ya kigeni.

Lakini wakati somo kuhusu Iraq linaanza kupatikana , Marekani inajaribu kutafuta ugonvi kwingine. Baada ya kutoleana maneno ya mvutano na Iran katika miezi ya hivi karibuni, sasa kwa kusema kweli kuna hatari ya risasi pia kufyatuliwa. Bush ameamua kuweka maroketi ya Patriot katika eneo la ghuba na ameamuru meli ya pili ya kubebea ndege kuwekwa katika eneo hilo la mizozo. Kwa hiyo si jambo la kawaida , wakati mtu yuko katika mazungumzo ya kisiasa na upande mwingine. Rais Bush anataka wazi kabisa kupambana kabla ya yeye kung’atuka na kustaafu, linaeleza gazeti la Märkische Oderzeitung.

Nae mhariri wa gazeti la Tageszeitung la Berlin akizungumzia suala hilo anatia shaka, kwamba wanajeshi wa Marekani siku ya Alhamis iliyopita katika mji wa kaskazini mwa Iraq wa Erbil walivamia wakala mmoja wa Iran na kuwakamata Wairan watano, na hali ya wasi wasi baina ya Iran na Marekani imeanza tena. Huu ni ushahidi kamili kuwa Marekani haijaacha kujaribu kulinda maslahi yake kwa nguvu katika eneo la mashariki ya kati. Kinyume chake kuongeza majeshi ya Marekani nchini Iraq pamoja na hali ya msuguano wa kimabavu na Iran na Syria , unaonyesha wazi kuwa njia hii ya kuleta majanga inayotumiwa na Marekani bado inaendelea kutumiwa.