1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhasama kati ya Fatah na Hamas waongezeka

Kalyango Siraj1 Agosti 2008

Kila kundi lakamata wafuasi wa kundi lingine katika eneo lake

https://p.dw.com/p/EoWi
Moja wa askari polisi wa Hamas akishika doria karibu na gari lililoharibiwa na bomu.Hamas inalinyooshea kidole kundi la Fatah.Lakini kundi hilo limekanusha kuhusikaPicha: AP

Vikosi vya usalama vya kundi la kipalestina lenye msimamo mkali la Hamas limewatia mbaroni wajumbe wa kundi lingine la Kipalestina linaloongozwa na mkuu wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas la Fatah.

Kamatakama hii inatokana na mlipuko wa bomu katika ukanda wa Gaza unaodhibitiwa na Hamas ambao uliwauwa wapiganaji watatu pamoja na msichana mmoja.

Makundi mawili ya kipalestina yanaendeleza uhasama baina ya makundi hayo .Mamlaka ya Palestina yanayoongoza Ukingo wa Magharibi pamoja na kundi la Hamas linalodhibiti ukanda wa Gaza, kila limoja linaendelea na kamatakamata ya viongozi wa kundi lingine katika eneo lao.

Mvutano mpya ambao umezusha kamata hizo umechochewa na mlipuko wa bomu lilikuwa limefichwa ndani ya gari. Mlipuko huo ambao ulitokea katika Ukanda wa Gaza sio tu ulimuua msichana mmoja lakini pia wapiganaji watano wa kundi la Hamas.

Kundi la Hamas linalilaumu kundi la Fatah kwa kuhusika na limefanya msakao na kuwaklamata watu wanaoonekana ni wafuasi wa kundi la Fatah.Miongoni mwa waliokamatwa ni wajumbe wa ngazi za juu wa kundi la Fatah katika ukanda wa Gaza.Wanausalama wa Hamas wamewakamata Ibrahim Abu an-naja pamoja na Zakaria al-Agha ambao waliteuliwa na rais Mahmoud Abbas kusimamia mali za Fatah katika eneo hilo baada ya wapiganaji wa Hamas kuchukua hatamu za Ukanda wa Gaza mwaka mmoja uliopita.

Msemaji wa kundi la Hamas Taher al-Nunu amekanusha madai ya kuwakamata watu kutokana na tofauti za kisiasa.

Lakini kundi la Fatah linakanusha kuhusika na kuongeza kuwa mlipuko huo ulisababishwa na mgawanyiko ndani ya kundi hilo la Hamas.

Ingawa jana alhamisi rais Mahmoud Abbas alikuwa ameviagiza vikosi vyake vya usalama kuwaachilia huru wafuasi wote wa Hamas waliokamatwa katika ukingo wa magharibi katika kipindi cha wiki moja hivi,lakini rubaa za karibu na waliokamatwa zimeliambia shirika la habari la Ujerumani la DPA leo Ijumaa kuwa wahana habari za kuachiliwa kwa mtu yoyote.

badala yake wanasema kuwa watu wengine wengi wamekamatwa usiku wa kuamukia leo Ijumaa.Miongoni mwa wanaemdai kukamatwa ni Muhammad Ghazal mjumbe wa baraza tawala wa Hamas pamoja na wanachama wengine wa kundi hilo katika ukingo wa magharibi.

Kundi la Hamas kupitia taarifa limesema kuwa viongozi wa Fatah walikamatwa kufuatia kukamatwa kwa wenzao.

Makundi haya mawili yamekuwa yakizozana tangu kundi la Hamas kulishinda la Fatah katika uchaguzi wa bunge uliofanyika januari mwaka wa 2006.Hali iliongezeka kuwa mbaya Juni mwaka wa 2007 wakati wapiganaji wa Hamas walipowafurusha wapiganaji watiifu kwa Mahmoud Abbas kutoka Ukanda wa Gaza.