1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhasimu wa riadha kudhihirika London

3 Agosti 2012

Baada ya wiki moja ya kusubiri tangu kuanza michezo ya Olimpiki, hatimaye vitengo vya riadha vilianza jana Ijumaa katika uwanja wa Olimpik jijini London. Ni fursa ya kuona uhasimu wa tangu jadi katika vitengo mbalimbali

https://p.dw.com/p/15jb1
epa02919720 Ethiopia's Kenenisa Bekele celebrates while crossing the finish line to win the men's 10,000m race at the Memorial Ivo Van Damme - Diamond League athletics meeting in Brussels, Belgium, 16 September 2011. EPA/YORICK JANSENS BELGIUM OUT +++(c) dpa - Bildfunk+++
Äthiopien Kenenisa BekelePicha: picture-alliance/dpa

likuwa fursa kwa wageni waliosafiri London kuuona kwa mara ya kwanza uwanja wa Olimpik wenye uwezo wa kuwa na mashabiki 80,000, tangu kufanyika sherehe ya ufunguzi. Na tangu jana ijumaa Mashabiki wa olimpiki wameendelea kufurika furi furi ndani ya treni za abiria na kupanga foleni ndefu katika vituo vya treni jinni London. Kufikia sasa mfumo huo wa uchukuzi umehimili hali hiyo ya mssongamano wa abiria tangu kuanza michezo ya Olimpiki, lakini kuanza kwa mashindano ya vitengo vya riadha kunatarajiwa kuwa mtihani mkubwa kwa miundo mbinu.

Maafisa wa uchukuzi jijini London wamewashauri abiria kutumia barabara nyingine mbadala baada ya barabara ya katikati ambayo huunganisha katikati ya jiji la London na uwanja wa Olimpik kufungwa kwa muda wa saa moja kutokana na hitilafu ya kiufundi.

Usafiri umekumbwa na changamoto kutokana na idadi kubwa ya abiria
Usafiri umekumbwa na changamoto kutokana na idadi kubwa ya abiriaPicha: dapd

Kesho Jumapili mwanariadha wa kenya Mary Keitany atalenga kutwaa medali ya dhahabu katika mbio za marathon upande wa kina dada. Keitany mwenye umri wa miaka 30 anayetafuta taji lake la kwanza la ubingwa wa kimataifa, anapigiwa upatu baada ya kuwa mwanamke wa tatu wa kasi zaidi katika kitengo hicho alipotimka mbio za London Marathon mwezi Aprili kwa kutumia mudaw a saa 2.18.37. Keitany anasema yuko katika hali nzuri na ana matumaini ya kufanya vyema. Kikosi cha kenya kina majina kama vile bingwa wa ulimwengu Edna

Kiplagat, na Priscah Jeptoo. Kenya imewahi kupata nishani ya fedha katika mbio hizo wakati Catherine Ndereba alipomaliza wa pili mnamo mwaka wa 2004 na 2008.

Kwingineko, Mwanariadha wa mbio za masafa mafupi Mjamaica Asafa Powell amewasilisha malalamiko kwa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki IOC baada ya kuamshwa kutoka usingizini ili kufanyiwa vipimo vya dawa zilizoharamishwa.

Usafiri umekumbwa na changamoto kutokana na idadi kubwa ya abiria
Usafiri umekumbwa na changamoto kutokana na idadi kubwa ya abiriaPicha: dapd

Meneja wa mwanariadha huyo wa mita mia moja, Pauk Doyle amesema Powell aliamshwa mwendo wa saa nne na robo usiku saa za London ili afanyiwe vipimo. Doyle alisema hawapingi kupimwa, lakini wanastahili kuheshimu maandalizi ya mwanariadha huyo. Aliongeza kwua ikiwa imesalia saa 48 tu, Powell alipoteza usingizi wake muhimu.

Tukiachana na michezo ya Olimpiki hebu sasa tuangazie mecho katika ulimwengu wa soka barani Ulaya ambapo wakati timu zikiendelea kufanya matayarisho ya mwisho mwisho ya kuanza misimu mipya ya ligi, klabu ya Arsenal imeripotiwa kupata saini ya mchezaji wa Uhispania Santiago Carzola kutoka klabu ya Malaga. Carzola alisema kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa yeye sasa ni mchezaji wa Arsenal.

Na hapa hapa Ujerumani, Mwanasoka wa Ubelgiji Kevin De Bruyne amejiunga na klabu ya Werder Bremen kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja. Klabu hiyo ya Ligi ya taifa ya Ujerumani Bundesliga imesema Alhamisi kuwa uhamisho huo hauna kipengee cha kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 De Bruyne kwa mkataba wa kudumu. Chipukizi huyo alijiunga na Chelsea kutoka klabu ya Racing Genk ya Ubelgiji mwezi Januari kisha akarejeshwa tena katika klabu hiyo kwa mkopo kwa kipindi kizima cha msimu uliopita.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA

Mhariri: Mohammed Khelef