1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUhispania

Uhispania yapanga kutuma mfumo wa ulinzi wa anga Ukraine

Amina Mjahid
26 Aprili 2024

Gazeti la serikali la Uhispania la El Pais, limesema nchi hiyo itatuma idadi ndogo ya mfumo wa ulinzi wa angani aina ya Patriot kwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4fDg0
Uhispania inapanga kutuma mfumo wa ulinzi wa anga aina ya Patriot nchini Ukraine
Uhispania inapanga kutuma mfumo wa ulinzi wa anga aina ya Patriot nchini Ukraine Picha: Kyodo/IMAGO

Gazeti la serikali la Uhispania la El Pais, limesema nchi hiyo itatuma idadi ndogo ya mfumo wa ulinzi wa angani aina ya Patriot kwa Ukraine kujibu shinikizo la kufanya kutuma msaada zaidi wa kijeshi kwa kiev lililotolewa na Umoja wa Ulaya pamoja na Jumuiya ya kujihami NATO.

Wakati Urusi ikizidisha mashambulizi yake kwa Ukraine, serikali za umoja huo zimehimizwa kuipa Kiev mifumo zaidi ya kujilinda, hasa Ugiriki na Uhispania walio na mifumo hiyo katika maghala yao ya silaha. Hata hivyo, Ugiriki imesema haitotuma mifumo hiyo nchini Ukraine.

Mapema mwezi huu Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy aliwaambia wanachama wa NATO kwamba nchi yake inahitaji mifumo takriban saba ya ulinzi wa anga au mifumo mengine ya hali ya juu ya kujilinda ili iweze kukabiliana na mashambulizi kutoka Urusi.

Ujerumani kwa upande wake imeahidi kuipa Ukraine mfumo mmoja wa ulinzi wa Patriot na kutaka mataifa mengine ya NATO kutoa mifumo mingine sita.