1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhispania, Morocco zawaangamiza wanamgambo wa IS

Sekione Kitojo
6 Septemba 2017

Majeshi ya Uhispania na Morocco yamelivunja kundi linalodaiwa kuwa na uhusiano na wanamgambo wanaojiita Dola la Kiislamu ambapo wanachama wake sita walikuwa wakifanya mafunzo na kupanga kufanya mashambulizi. 

https://p.dw.com/p/2jQtK
Marokko Casablanca, Reportage Umfeld Vergewaltigung | Al-Bernoussi Stadtviertel
Picha: DW/I. Talbi

Wizara ya mambo ya ndani ya Morocco inasema kwamba watu watano walikamtwa karibu na mji wa kaskazini wa Morocco wa Nador na mmoja alikamatwa karibu na eneo la Uhispania la Melilla,

Kukamatwa huko kumekuja wiki kadhaa baada ya mashambulizi yaliyofanywa na watu wenye itikadi kali nchini Uhispania wakiwa na mahusiano na Morocco, ambapo watu 16 waliuwawa mjini Barcelona.

Watano kati ya watu hao waliokamatwa leo (Septemba 6) ni Wamorocco na mmoja ni Mhispania mwenye asili ya Morocco, imesema wizara ya mambo ya ndani ya Uhispania.

Kiongozi wa kundi hilo lililovunjwa ana umri wa miaka 39 anayeishi Melilla ambaye alikamatwa wakati akitembelea Morocco.