1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhusiano kati ya Ujerumani na Ufaransa waimarika

24 Septemba 2012

Uhusiano kati ya Ujerumani na Ufaransa na nani ateuliwe na SPD kupigania kiti cha kansela katika uchaguzi mkuu mwakani ni miongoni mwa mada zilizochambuliwa zaidi na wahariri wa magazeti ya Ujerumani.

https://p.dw.com/p/16DFt
Rais wa Ufaransa Francois Hollande na mwenyeji wake kansela Angela Merkel wakati wa mkutano wao huko LudwigsburgPicha: dapd

Tuanze na mkutano wa mwishoni mwa wiki kati ya kansela Angela Merkel na rais Francois Hollande wa Ufaransa katika mji wa kusini magharibi wa Ludwigsburg.Wasi wasi uhusiano kati ya Ufaransa na Ujerumani usije ukadhoofika baada ya kuingia rais mpya katika kasri la Elysée umefifia.Gazeti la "Ludwigburger Kreiszeitung" linaandika:

Angela Merkel ambae ni Mwana-Christian Democratic na Francois Hollande ambae ni msoshilisti wanajitahidi kujongeleana.Wote wawili wanafuata siasa za kufikia maridhiano wakitanguliza mbele matokeo ya majadiliano yaliyofanyika kwa njia ya usawa.Kwamba Angela Merkel ameshaanza kulitaja neno "urafiki",katika wakati ambapo Francois Hollande neno hilo bado hajaanza kulitumia,si tatizo.Kiongozi huyo wa Ufaransa ndio kwanza ameingia madarakani, kwa hivyo anahitaji muda kidogo kuweza kuuingilia uwanja huo.

Francois Hollande Angela Merkel Ludwigsburg 2012
RaisFrancois Hollande na kansela Angela MerkelPicha: THOMAS KIENZLE/AFP/GettyImages

Gazeti la "Westdeutsche Zeitung" linahisi "hakuna badala ya Merkel na Hollande.Gazeti linaendelea kuandika:

Historia ya uhusiano kati ya Ujerumani na Ufaransa ni ya kusisimua.Tuchukue mfano wa Valery Giscard d'Esteing na Helmut Schmidt.Francois Mitterand na Helmut Kohl,Jacques Chirac na Gergard Schröder au Nicolas Sarkozy na Angela Merkel.Mivutano ya ndani,mikondo tofauti ya kisiasa na hata dhana za kutoweza kusikilizana,zimeweza kutoweka.Wakosoaji wanaweza kusema "ni unafik huo.Muhimu lakini ni kwamba tabia hiyo imesaidia kuimarisha fikra uhusiano mzuri wa mataifa haya mawili ndio msingi wa Umoja madhubuti wa Ulaya.Hata kama bado kuna mambo ambayo misimamo ya kansela Angela Merkel na Francois Hollande hailingani ,lakini la muhimu wameanza kujongeleana.Alikuwa Francois Hollande aliyetamka huko Ludwigsburg" nchi zetu mbili ndio moyo wa Ulaya."Hajakosea."

SPD Sigmar Gabriel Frank-Walter Steinmeier Peer Steinbrück Zukunftskongress Berlin Deutschland
Eti nani kati ya Sigmar Gabriel(kati) Frank-Walter Steinmeier(kulia) na Peer Steinbrück (kushoto) akiongoze chama cha SPD katika uchaguzi mkuu mwakani?Picha: picture-alliance/dpa

Mwaka mmoja kabla uchaguzi mkuu kuitishwa nchini Ujerumani,homa imeshaanza kupanda miongoni mwa wanasiasa,na hasa wa upande wa upinzani wa Social Democratic na walinzi wa mazingira Die Grüne waliamua kuwaaachia wanachama mikoani waamue nani aongoze orodha ya chama chao.Kishindo kikubwa zaidi kinakikaba chama cha Social Democratic linaandika gazeti la "Saabrücker Zeitung".

Suala la nani awe mgombea wa kiti cha kansela kwa tikiti ya chama cha Social Democratic limehanikiza kila pembe.Hapapiti siku bila ya kuzuka uvumi,eti suala hilo halizuki tena kwasababu wana SPD wameshaamua.Kwamba wasoshial Democratic kwa kufanya hivyo wanawaudhi wapiga kura,si siri kwa yeyote yule.Pengine wasia wa mwana CSu,Theo Waigel utawasaidia:Anawashauri wote watatu washindane na Angela Merkel,na baadae ndo achaguliwe anaestahiki kuwa kansela kati yao.Ni mzaha bila ya shaka,lakini ikiwa SPD itaendelea kuzozana kuhusu suala hilo,kitakachowasalia pengine ni nafasi ya kuchaguliwa kuwa makamo kansela.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri :Yusuf Saumu