1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Uingereza kuionya Israel kuhusu njaa katika ukanda wa Gaza

Tatu Karema
6 Machi 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Cameron amesema nchi yake itaionya Israel kwamba uvumilivu wake unapungua kuhusu mateso ya kutisha katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4dDU1
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Cameron
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David CameronPicha: THOMAS KIENZLE/AFP

Kauli ya Cameron inatokea katika wakati ambapo ukosefu wa misaada unasababisha watu kufa kutokana na njaa katika ukanda wa Gaza.

Cameron ambaye anatarajiwa kukutana na mjumbe wa baraza la mawaziri la vita la Israel Benny Gantz hii leo, ameliambia bunge la Uingereza jana jioni kwamba jinsi Israeli inavyoshughulikia misaada ya wakaazi wa Gaza, inaibua maswali kuhusu uzingatiaji wake wa sheria za kimataifa.

Soma pia: Hamas yaahidi kuendelea na mazungumzo hadi makubaliano

Cameron ameliambia bunge hilo kwamba wiki kadhaa zilizopita alizungumzia kuhusu hatari ya kuzuka kwa baa la njaa na magonjwa na sasa hali imefikia kiwango hicho.

Waziri huyo ameongeza kuwa watu wanakufa kutokana na njaa na magonjwa yanayoweza kuzuilika.

Cameron ameliambia bunge hilo kwamba  msaada uliopelekwa Gaza mwezi Februari ulikuwa karibu nusu ya kiwango kilichotolewa mwezi Januari.