1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza yazidi kuilipa Rwanda

Grace Kabogo
8 Desemba 2023

Uingereza iliilipa Rwanda pauni milioni 100 zaidi mwezi Aprili, mbali na pauni milioni 140 ambazo tayari zilitolewa mwaka uliopita.

https://p.dw.com/p/4Zwat
Waandamanaji wakipinga makubaliano ya Uingereza na Rwanda kuhusu waomba hifadhi.
Waandamanaji wakipinga makubaliano ya Uingereza na Rwanda kuhusu waomba hifadhi.Picha: Vuk Valcic/Zuma Wire/IMAGO

Hayo yameelezwa na wizara ya mambo ya ndani, na kwamba fedha hizo zililipwa kabla hata kabla ya waomba hifadhi kuondolewa nchini humo.

Wizara hiyo imesema malipo hayo ambayo awali hayakuwekwa wazi, yalikubaliwa mwezi Aprili mwaka huu chini ya mfuko wa maendeleo ya kiuchumi na ukuaji wa Rwanda.

Soma zaidi: Mahakama Uingereza yabatilisha kupeleka wakimbizi Rwanda

Serikali ya Uingereza iliongeza kuwa inatarajia kutoa pauni milioni 50 zaidi mwaka ujao kwa Rwanda kama sehemu ya mfuko huo huo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rwanda haikuomba malipo yoyote ili makubaliano mapya yasainiwe, kwa lengo la kuufufua mpango wa serikali ya Uingereza kuwapeleka watu wanaoomba hifadhi kwenye nchi hiyo ya Afrika Mashariki.