1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujeruamani yasema imepokea habari za onyo la shambulio la kigaidi

13 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Coxy

BERLIN:

SERIKALI YA Ujerumani inasema imepokea onyo kutoka kwa wakuu wa Lebanon kuwa watu wenye imani kali wanapanga kufanya shambulizi la kigaidi nchini Ujerumani.Maafisa wanasema wamepewa tahadhari hiyo baada ya maafisa wa Lebanon kumkamata mtu mmoja anaeshukiwa ni mshirika wa kundi la kigaidi la al-Qaida mjini Beirut.Mtuhumiwa huyo anaaminika kuwa ameupigia simu ubalozi wa Ujerumani mjini Beirut mapema wiki hii.akidaiwa kuwa ametishia kufanya shambulizi katika maeneo ya kiusalama ya Ujeruamni kwa kulipiza kisasi kwa ajili ya kuhukumiwa mtuhumiwa wa kundi la al-qaida nchini Ujerumani.