1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani-Dhima ya vyama vidogo katika serikali ya muungano

21 Septemba 2009

Chama cha kiliberali FDP, kinataka kushirikiana na vyama vya kihafidhina vya CDU/CSU kuunda serikali ya muungano kufuatia uchaguzi mkuu wa Ujerumani utakaofanyika Septemba 27.

https://p.dw.com/p/JlVV
Der FDP-Vorsitzende Guido Westerwelle spricht am Montag, 8. Juni 2009, in Berlin auf der Pressekonferenz nach der Europawahl. (AP Photo/Fritz Reiss) --German Liberal party FDP chairman Guido Westerwelle delivers a press statements during a news conference after the European elections in Berlin on Monday, June 8, 2009. (AP Photo/Fritz Reiss)
Mwenyekiti wa chama cha kiliberali FDP-Gudio Westerwelle.Picha: AP

Uamuzi huo ulipitishwa kwa kauli moja na chama cha FDP katika mkutano wake siku ya Jumapili mjini Potsdam. Kiongozi wa chama cha kiliberali cha FDP Guido Westerwelle amesema waziwazi kuwa chama chake hakitoshirikiana na Social Democratic SPD na chama cha Kijani kuunda serikali ya muungano. Amesema:

"Bila ya kusitasita tumeamua kushirikiana na CDU kwa sababu mipango ya SPD na chama cha KIjani itawapa wananchi mzigo mkubwa na itaathiri viwanda. Hayo ni kinyume na dhima ya FDP."

Uchunguzi wa maoni uliofanywa siku za hivi karibuni umeashiria kuwa chama cha kihafidhina CDU cha Kansela Angela Merkel na cha waliberali FDP huenda vikapata wingi mdogo bungeni na kuweza kuunda serikali ya muungano yenye sera za wastani za mrengo wa kulia baada ya uchaguzi wa Jumapili ijayo.

Serikali kama hiyo huenda ikajaribu kushusha kodi ya mapato, kupunguza udhibiti wa serikali katika sekta ya uchumi na kuendelea kutumia viwanda vya nyuklia kuzalisha nishati na hali imeshakubaliwa kuvifunga viwanda vya nyuklia nchini Ujerumani,hatua kwa hatua katika kipindi cha miaka kumi ijayo.Chama cha Kijani kinatuhumu kuwa CDU na FDP vilikuwa na mpango wa kujenga mitambo ya nishati ya nyuklia kwa siri na hata kupunguza usaidizi wa fedha kwa wanyonge.Hata hivyo,chama cha Kijani hakiamini kuwa FDP kitangángania msimamo wake wa kutaka kushirikiana na CDU/CSU tu ikiwa CDU na FDP havitofanikiwa kujikingia kura za kutosha katika uchaguzi ujao ili kuweza kuunda serikali ya muungano.

Kwa upande mwingine, njia pekee kwa mgombea ukansela wa chama cha SPD Waziri wa Mambo ya Nje Frank-Walter Steinmeier kushika wadhifa huo ni kwa vyama vya FDP,Kijani na SPD kushirikiana katika serikali ya muungano.

ARCHIV - Die Spitzenkandidatin der Gruenen fuer die Bundestagswahl Renate Kuenast, spricht am 31. August 2009, nach einer Parteiratssitzung in Berlin zu Journalisten. Kuenast, hat den nordrhein-westfaelischen Ministerpraesidenten Juergen Ruettgers (CDU) als Rassisten bezeichnet. Sie forderte in der "Leipziger Volkszeitung" in deren Ausgabe fuer Montag, 7. September 2009, die CDU-Chefin und Bundeskanzlerin Angela Merkel auf, sich von Ruettgers als stellvertretendem Parteivorsitzenden zu trennen. Hintergrund sind die juengsten Aeusserungen des Duesseldorfer Regierungschefs ueber rumaenische Arbeiter und chinesische Investoren. (AP Photo/Markus Schreiber, Archiv) ** zu APD4327 ** --- FILE - In this Aug. 31, 2009 file photo Germany's Green Party top candidate for the upcoming general elections Renate Kuenast briefs the media after a Green Party leaders meeting in Berlin, Germany. (AP Photo/Markus Schreiber, File)
Renate Künast. mgombea mkuu wa chama cha Kijani.Picha: AP

Renate Künast wa chama cha Kijani kinachotaka kuzuia serikali ya muungano wa vyama vya CDU/CSU na FDP amesema:

" Kila anaemtaka Steinmeier kuwa kansela nchini humu, basi Jumapili ijayo aitumie kura yake ya pili kukipigia chama cha Kijani ama sivyo mpango huo utavurugika."

Ikiwa Merkel hatofanikiwa kupata kura za kutosha ili kuweza kuunda serikali pamoja na FDP basi kuna uwezekano mwingine - kuendelea na serikali ya muungano wa vyama vikuu pamoja na SPD anayoiongoza tangu mwaka 2005. Lakini Merkel na Steinmeier katika kampeni zao za uchaguzi wameshasema kuwa wasingependa kuendelea na muungano huo licha ya kuweza kutekeleza mambo mengi wakati wa miaka minne iliyopita.

Mwandishi: P.Martin/DPA

Mhariri: M.Abdul-Rahman