1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani imeahidi msaada zaidi kwa wahanga wa ukame

Mnette,Sudi/dpae16 Julai 2011

Serikali ya Ujerumani imeongeza msaada wake kwa zaidi ya maradufu kwa ajili ya watu wanaokimbia ukame katika eneo la Pembe ya Afrika.

https://p.dw.com/p/RaFn
Somalis women and children from southern Mogadishu, line up to receive food at a camp in Mogadishu distributed by Jumbo organization a local NGO in Mogadishu , Somalia, after fleeing from southern Somalia, Thursday, July 7, 2011. Thousands of people have arrived in Mogadishu over the past two weeks seeking assistance and the number is increasing by the day, due to lack of water and food. The worst drought in the Horn of Africa has sparked a severe food crisis and high malnutrition rates, with parts of Kenya and Somalia experiencing pre-famine conditions, the United Nations has said. More than 10 million people are now affected in drought-stricken areas of Djibouti, Ethiopia, Kenya, Somalia and Uganda and the situation is deteriorating, (AP Photo Farah Abdi Warsameh)
Wahanga wa ukame katika Pembe ya AfrikaPicha: dapd

Msaada huo wa euro milioni 5, utatumiwa kuwashughulikia wakimbizi katika maeneo yaliyoathirika zaidi. Mashirika ya misaada yamekadiria kuwa kiasi ya watu milioni 10 wanakabiliwa na kitisho cha njaa.

Kenyan President, Mwai Kibaki, left, and the Chancellor of the Federal Republic of Germany, Angela Merkel, stand at attention during a welcoming ceremony at State House Nairobi, Tuesday July 12, 2011, on the first day of her two-day official visit to Kenya. (Foto:Khalil Senosi/AP/dapd)
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel(kushoto) na Rais wa Kenya Mwai KibakiPicha: dapd

Wizara ya misaada na wizara ya mambo ya nje, zimesema kuwa msaada huo wa serikali ya Ujerumani, utagawanywa miongoni mwa mashirika ya misaada ya Ujerumani na mataifa mengine pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula-WFP.

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, alitembelea Kenya jumanne iliyopita ambapo aliahidi msaada wa euro milioni 1 kwa ajili ya kambi za wakimbizi. Nusu ya msaada huo,ilitengwa kwa ajili ya matumizi ya dharura ya WFP.