1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani ina miadi leo na Ghana

23 Juni 2010

Algeria itaaga nayo leo Kombe la dunia kwa heshima ?

https://p.dw.com/p/O0lc
Schweinsteiger na Podolski wajinoa kabla zahama na Ghana.Picha: picture alliance / dpa

Baada ya jana wenyeji wa Kombe la Dunia 2010 ,Bafana bafana kuaga na mapema duru ya kwanza Kombe la Dunia, na kufuata mkondo ulioanzishwa na Kameroun,Ivory Coast na jana Nigeria,leo ni zamu ya Black Stars- Ghana,kujua hatima yake , ikipambana na mabingwa mara 3 wa dunia-Ujerumani.Kama Ghana, Ujerumani, lazima ishinde leo usiku ili kubakia mashindanoni. Alaasiri ya leo, mpambano huo utatanguliwa na changamoto kati ya Algeria na Marekani, na Uingereza na Slovenia. Marekani lazima ishinde ili iifuate ama Slovenia au Uingereza duru ijayo.

UJERUMANI NA GHANA LEO

Ujerumani nzima inasubiri ka shauku kuu,mpambano wa usiku wa leo kati ya Black Stars -Ghana na Ujerumani.Kwanza, Ujerumani lazima ishinde ikiwa ibakie katika Kombe la dunia.Pili,Ujerumani ina kisasi kingine kwa Ghana:Ni mzaliwa wa Ujerumani ,mchezaji wa kiungo wa Ghana,Kevin-Prince Boateng, aliemuumiza Ballack wakati wa finali ya Kombe la FA kati ya Chelsea na Portsmouth na kumpiga kumbo nje ya mpambano wa leo.

Ndugu 2:Kevin-Prince Boateng na Jerome Boteng,wanachezea timu 2 hasimu:mmoja Ghana mwengine Ujerumani. Ni pili pili hoho hizo ziklo nyuma ya mpambano wa leo.Je, Ghana, itaitilia Ujerumani kitumbua chake mchanga ? Au Ujerumani itaisindikiza Ghana nyumbani kufuata nduguze watano.

ALGERIA NA MAREKANI

Kabla ya Ujerumani kucheza na Ghana, Algeria ina miadi na Marekani.Marekani lazima ishinde .Algeria ina pointi 1 kwa kutoka suluhu na Uingereza.TZimu hizi mbili hazikuwahi kukutana na hii leo itakua mara ya kwanza .mambo yatakuaje ? Je, Algeria, itaaga Kombe la dunia kwa heshima kama Bafana bafana jana ?

Kocha wa Ufaransa,Reymond Domenech,hatima yake inajulikana.Si kocha tena wa Ufaransa,baada ya kikosi chake kuiabisha Ufaransa nzima.Kocha mpya alikwisha chaguliwa hata kabla ya Kombe hili la dunia.Laurent Blanc,alietawazwa bingwa wa dunia pamoja na Zinedine Zedane, 1998 nyumbani Ufaransa.

Kocha Domench,aliwasangaza mashabiki jana alipokataa kuupokea mkono wa kocha wa Bafana Bafana,mbrazil Luoius Parreira.Kisa nini ?

Sababu ni kuwa,Parreia,pale Ufaransa ilipokata tiketi yake ya Kombe hilila dunia kwa bao la mkono la nahodha wake wazamani Thierry Henry, alisema "Afrika Kusini,haikustahiki kuja kwenye Kombe la Dunia."

Hii ilimuudhi kocha Domench, na kwahivyo, hakutaka mkono wa Parreira.

Mwandishi: Ali Ramadhan /AFPE

Mwandishi: Abdul-Rahman