1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani inakabiliana na tatizo wanafunzi wengi

14 Julai 2017

Utafiti mpya nchini Ujerumani umetabiri kuongezeka kwa wanafunzi kwa sababu ya kuongezeka kwa watoto wahamiaji na kupanda kwa kasi viwango vya kuzaa.

https://p.dw.com/p/2gZZn
Deutschland junge Flüchtlinge - Integration
Picha: Getty Images/S. Gallup

 Utafiti mpya nchini Ujerumani umetabiri kuongezeka kwa wanafunzi kwa sababu ya kuongezeka kwa watoto wahamiaji na kupanda kwa kasi viwango vya kuzaa. Muandishi wa utafiti huoa naonya kuwa hawajajipanga kukubiliana na changamoto hiyo. Mbali na  makadirio yaliyotabiri kushuka kwa idadi ya wanafunzi katika shule za Ujerumani kwa siku za usoni - kulingana na utafiti mpya wa wakfu wa  Bertelsmann unaonesha  kinyume chake kinawezekana kutokea.

Wimbi kubwa la wale waliostaafu, kutokuwepo kwa walimu wapya, kuongezeka kwa wanafunzi na upungufu madarasa, waandishi wa sheria wanapaswa kurekebisha haraka mipango ya shule na elimu, anasema Dirk Zorn, msimamaizi wa  wa Bertelsmann.

Kwa mujibu wa utafiti huo, uliochapishwa Jumatano, shule za Ujerumani zinaweza kutarajia zaidi ya wanafunzi milioni 1 zaidi ya kufikia  2025 ikilinganishwa na idadi zilizotabiriwa mwaka 2013 na Kamati ya Kudumu ya Mawaziri wa Utamaduni wa Ujerumani.

Kiwango cha kuzaa kwa Ujerumani ambalo kilikuwa cha chini sana duniani kwa miongo kadhaa - kimeongezeka kwa miaka mitano iliyopita. Hii, pamoja na mvuto wa wahamiaji ni sababu kuu za kuongezeka kwa wanafunzi  katika kipindi cha miaka minane, alisema Zorn, akiongeza  kusema kuwa hili ni ongezeko kubwa la watu.

Katika mwaka wa shule wa  2015/2016, wanafunzi milioni 7.9 wamejiunga na shulle Ujerumani kote.

2025 ambao hauko mbali sana, utafiti wa Bertelsmann unatarajia kuwepo kwa  wanafunzi milioni 8.3, kiasi kikubwa zaidi kuliko ilipokadiriwa  hapo awali na Kamati ya Kudumu ya Mawaziri wa Utamaduni wa Ujerumani.

Kwanini Ujerumani haijajipanga

Schweigeminute in den deutschen Schulen
Picha: AP

Lakini kwanini Ujerumani, haijajipanga kupambana na tatizo hili? Hapo awali  shule ziliambiwa watarajie nambari za wanafunzi wanaojiunga na shule kushuka, lakini utafiti huo mpya serikali ya shirikisho anatarajiwa kuwekeza kama  euro billioni 4.7 kwa mwaka kuepuka upungufu mkubwa wa walimu na madarasa katika mashule.

Zorn alisema wakati wakutarajia nambari za wanafunzi kushuka umekwisha.

Idadi ya watoto katika shule ya msingi inatarajiwa kuongezeka kutoka milioni 2.8 mwaka 2015 hadi milioni 3.2 mwaka 2030. Miaka minane kutoka leo, shule za msingi za Ujerumani zinaweza kuwa na upungufu wa hadi waalimu 24,000, hali ambayo pia itazikumba shule za juu, ambazo tayari zinakabiliana na wimbi la walimu wanaostaafu na ukosefu wa walimu vijana.

Mwenyekiti wa Chama cha walimu mjini Berlin, Udo Beckmann amesema kuwa hayo ni makadirio yanayokubalika, ameongezea kusema pia kuwa wanasiasa wamekuwa wakilipuuza swala la upungufu wa walimu kwa muda mrefu sana. mwenyekiti huyo alisema pia kuwa Kamati ya Kudumu ya Mawaziri wa Utamaduni wa Ujerumani, imekuwa ikitoa makadirio yaliokuwa sio sahihi.

Mwandishi: Najma Said

Mhariri      :  Daniel Gakuba