1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani injini ya Ulaya, asema Merkel

30 Januari 2014

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wameangazia zaidi leo (30.01.2014) katika hotuba aliyoitoa kansela Angela Merkel bungeni jana, pamoja na hotuba ya rais Barack Obama kuhusu hali ya taifa la Marekani.

https://p.dw.com/p/1AzQR
Angela Merkel Regierungserklärung 29.01.2014
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani akiwa bungeniPicha: Getty Images

Gazeti la Berliner Morgenpost , linaandika ni sawa kwa kansela aliposema katika hotuba yake bungeni jana kuwa anataka kuiweka Ujerumani kuwa injini ya Ulaya.

Lakini mtu hahitaji kuwa mtaalamu kuweza kutambua , kwamba injini ni pale tu inapoweza kufanyakazi kwa muda mrefu vizuri, na kwamba inatunzwa vizuri. Wakati inazeeka , inabidi pia kutarajia matatizo makubwa na madogo wakati ikiharibika.

Uzoefu

Uzoefu ambao pia unapatikana katika masuala ya kisiasa. Ujumbe wa Angela Merkel kutoka katika serikali yake ya mseto unazungumzia kuhusu ujenzi wa pamoja wa vyama vilivyomo katika serikali hiyo kuhusu mageuzi yenye tahadhari, ambayo Ujerumani inataka kuyatumia ili kujiimarisha.

Lakini hilo linabaki tamko lisilokuwa na nguvu, kwa kuwa linatibu tu dalili na kuwahudumia wateja maalum. Iwapo kuna ushahidi wowote wa maana , kwamba kuna watu wengi wanaoweza kuleta hali ya usalama wa hapo baadaye na kuondoa matatizo, serikali ya muungano mkuu ya kansela Merkel basi itaweza kuleta ufanisi.

Mhariri wa gazeti la Stuttgarter Zeitung anauliza je hiyo ilikuwa hotuba ya ripoti mpya? Iliyokusudiwa kwa ajili ya kuelezea kuhusu serikali hiyo mpya, vipi atakavyoiongoza chini ya Muungano huo? Au kansela Merkel amechota kutoka katika maelezo yaliyoandikwa na chama chake na kile cha kiliberali cha FDP?

Sawa, ni kweli kwamba katika msisitizo wa masuala ya kijamii amelenga katika kuimarisha utaratibu mpya. Na hata changamoto ya mabadiliko ya upatikanaji wa nishati ameonesha msimamo imara. Pamoja na hayo hakuna msukumo mpya, hakuna msisitizo maalum.

Kwa jumla hakuna suala muhimu kuhusu Ulaya na kuna ukosoaji wa kiasi tu katika kashfa ya udukuzi iliyofanywa na shirika la usalama wa taifa la Marekani NSA. Inabakia hali ya kujiuliza , tunaelekea wapi katika safari hii wakati tukielekea katika njia panda nyingine. Merkel , mhariri anaandika, kwa wastani anaendelea kubaki kuwa mwanamke tu.

Nalo gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung akizungumzia mada hiyo anaandika.

Mtandao wa internet utaendelea kuwa matumaini ya baadaye, amesema kansela Merkel katika hotuba yake bungeni jana. Lakini anauhusiano gani na matumaini haya ya baadaye? Kwa matamshi haya anatoa kansela kauli mbiu hatimaye katika kipindi chake cha tatu cha utawala, kwamba kwa hali yoyote ile iwayo hataweka vizuwizi katika matumizi ya mtandao.

Kwa kuwa uongozi huu umegundua kwa pamoja kuwa uwezo wa kiuchumi unahusiana pia na ufahamu wa jamii wa masuala ya kidemokrasia. Mambo haya yanahusiana pia na uchumi wa masoko nchini humu na serikali ya muungano inatambua kuwa ni jambo la kulikumbatia.

Mhariri wa gazeti la Die Welt anazungumzia hotuba ya rais Barack Obama kuhusu hali ya taifa la Marekani.

Ilikuwa ni hotuba ya sita ya Barack Obama kuhusu hali ya taifa la Marekani na hisia za mwanzo zinaonesha kuwa inaelekea katika njia ambayo tunaifahamu. Ukiangalia tena lakini utaona tofauti kuhusu hotuba hii na zilizopita za marais wa nchi hiyo wa zamani. Inaonesha wazi katika muktadha wake kile kinachokosekana.

Amesema hataongeza kodi kwa watu wenye kipato cha juu, Warepublikan hawajamuweka katika nafasi ngumu kutokana na kusita kwake kufanya mageuzi kuhusu haki ya wahamiaji na Obama amejiepusha pia na kuonesha kushangiria ushindi katika mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la al-Qaeda. Rais Obama ameoka mkate mdogo tu, kwasababu , miaka mitano baada ya kuingia madarakani , ametambua kwamba dunia haifanyikazi kama anavyotaka.

Lakini sasa unamfuata sasa mzigo wa kiapo chake anapokaribia mwisho wa uongozi wake. Wamarekani wanamuita bata kiwete.

Mwandishi: Sekione Kitojo / inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul Rahman