1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani itachangia maafisa wa polisi 180 Kosovo

6 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DJqt

BERLIN:

Ujerumani imekubali kuchangia maafisa wa polisi 180 katika kikosi maalum cha polisi na wataalamu wa kisheria cha Umoja wa Ulaya EULEX kitakachopelekwa Kosovo.Uamuzi huo umepitishwa kwenye mkutano wa baraza la mawaziri la Kansela Angela Merkel mjini Berlin.Kikosi hicho kitakuwa na kama maafisa 1,800.Niongoni mwao ni maafisa wa polisi 1,400.Wengine watakuwa maafisa wa sheria na forodha.

Lengo la ujumbe huo ni kuisaidia Kosovo kuunda serikali yake baada ya kujitangazia uhuru kutoka Serbia mwezi uliopita.Serbia inapinga ujumbe huo na inaendelea kudai kuwa ina mamlaka katika eneo hilo la Kosovo.