1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kuanza tena ushirikiano na shirika la UNRWA

24 Aprili 2024

Serikali ya Ujerumani inapanga kuanzisha tena ushirikiano wake na shirika la Umoja wa Mataifa, la kuhudumia wakimbizi Wakipalestina UNRWA katika ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4f7kC
Mgogoro wa Mahsriki ya kati
UNRWA: Ni shirika la Umoja wa Mataifa, la kuhudumia wakimbizi Wakipalestina UNRWA Picha: Mahmoud Issa/ZUMAPRESS/picture alliance

Haya ni kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa na ofisi ya wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani pamoja na wizara ya ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo.

Uamuzi huo unafuatia uchunguzi uliofanywa na waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Ufaransa  Catherine Colonna, kuhusu madai ya Israel kwamba baadhi ya wafanyakazi wa UNRWA walihusika katika shambulio la Oktoba 7 dhidi ya nchi hiyo.

Ripoti ya Colonna yasema Israel haijatowa ushahidi kuhusu tuhuma za kuwahusisha wafanyakazi wa UNRWA na shambulio la Oktoba 7

Uchunguzi huo usioegemea upande wowote siku ya Jumatatu ulihitimishwa kwa ripoti iliyobaini kwamba  Israeli haikuwa na ushahidi wowote kuthibitisha madai yake.

Wizara za Ujerumani zimehimiza shirika la UNRWA kutekeleza haraka mapendekezo ya ripoti hiyo ya uchunguzi, ikiwa ni pamoja na kuimarisha ukaguzi wa ndani na kuboresha usimamizi wa nje wa  miradi yake.