1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kuifundisha dunia jinsi ya kutunza mazingira

3 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVtF

BERLIN.Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa nchi yake itayakinisha harakati zake za kutunza mazingira katika mkutano wa mazingira unaoanza leo nchini Indonesia.Ujerumani ni nchi inayoongoza katika utunzaji wa mazingira duniani.

Kansela Merkel amesema kuwa Ujerumani itawasilisha mikakati ambayo itapelekea kupunguzwa kwa asilimia 40 ya utoaji wa gesi ya carbon ifikapo mwaka 2020.

Pia amesema kuwa Ujerumani itawasilisha mipango ya kupanua zaidi uzalishaji na utumiaji wa nishati mbadala.

Mkutano huo wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya hewa duniani, unahudhuriwa na wajumbe kutoka nchi 190 na unatarajiwa kuchukua kipindi cha wiki mbili ukijadili kwa kina jinsi ya kupambana na ongezeko la ujoto duniani.