1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kuisaidia Mamlaka ya Wapalestina

19 Mei 2010

Ziara ya waziri-mkuu Fayyad Berlin.

https://p.dw.com/p/NRgK
Salam Fayyad (kushoto) na Guido Westerwelle .Picha: AP

Waziri-mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya wapalestina, Salam Fayyad, alizuru jana Ujerumani na kuwa na mazungumzo mjini Berlin na serikali ya Ujerumani.Alishiriki pia katika kikao cha kwanza kabisa cha Halmashauri ya pamoja kati ya Ujerumani na Palestina.Waziri wa nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle,akamuahidi msaada wa Ujerumani kwa Mamlaka ya Ndani ya wapalestina.

Kwa mara ya kwanza kabisa imekutana mjini Berlin jana Halmashauri ya pamoja ya kuongoza ushirikiano kati ya Ujerumani na wapalestina .Mawaziri 10 kutika kila upande walishiriki katika kikao hicho ambacho siku zijazo kitafanyika mara moja kila mwaka.Mara moja Berlin na nyengine mjini Ramallah.

Waziri wa nje wa Ujerumani,Guido Westerwelle,aliona fahari kidogo juu ya aina hii mpya ya ushirikiano na Mamlaka ya Ndani ya Wapalestina.Akasema,

"Hiki ni kitu jipya kabisa.Kwani, mamlaka ya Ndani ya wapalestina haina jukwaa la mazungumzo pamoja na nchi yeyote nyengine ambamo mawaziri wa pande zote mbili , waweza kushauriana juu ujenzi na kuziendeleza ardhi za wapalestina. Tumepiga hatua hii kwavil, tunaamini kwamba maendeleo na hasa ujenzi wa Taasisi za dola katika ardhi za wapalestina, yanahitajika mno ili iwezekane kufikiwa suluhisho la haki la dola mbili katika Mashariki ya Kati."

Ujerumani inaungamkono mpango wa waziri-mkuu wa Palestina Salam Fayyad wa kujenga msingi wa taasisi tangui za kiuchumi hata za kisiasa za dola la wapalestina , na ndio maana itaongeza msaada wake kwa Utawala wa Ndani wa Wapalestina.

Bw.Westerwelle akaongeza,

"Kwa shabaha hiyo, tunaongeza msaada wetu wa maendeleo kwa kima cha Euro milioni 20 na Euro milioni 2 nyengine , kwa misaada ya kibinadamu,kujenga kikosi cha polisi huko Ukingo wa Magharibi,tunaongeza kima cha juu cha dhamana za mikopo kwa Hermes Bank,tunapanga kuwa na kituo maalumu cha uchumi Ukingo wa Magharibi pamoja na kuwasaidia na kuwaendeleza mbele wataalamu wa kisayansi wa kipalestina."

Waziri-mkuu Salam Fayyad, ana azma hadi ifikapo mwaka ujao 2011 kutangaza dola la wapalestina, endapo mazungumzo na Israel hadi wakati huo, bado yamekwama.Kwa shabaha hiyo, kupitia ujenzi wa taasisi za dola na raslimali, anataka aweze kuweka tayari miundo mbinu ya dola hilo.

Rais Mahmoud Abbas, wa Mamlaka ya Ndani ya wapalestina ,karibuni hivi aliupinga mapango huo wa kutangaza dola la wapalestina hivi karibuni wakati wa mahojiano na kituo cha TV cha Israel .

Kuna pia shaka shaka juu ya mradi huo wa waziri mkuu Fayyad.Wanaomkosoa wanadai kwamba, kwa kujenga barabara na mji mpya katika huko Ukingo wa Magharibi ,anaitua Israel na jukumu lake la dhamana zake kama dola linaloikalia sehemu hiyo.Lakini, waziri mkuu Fayyad , anahisi ni pale tu wapalestina watakapokuwa tena na matumaini ,ndipo watakapoweza kumaliza mgawanyiko kati yao.

Mwandishi: Marx,Bettina (DW Berlin)/Ramadhan Ali

Mhariri:Abdul-Rahman