1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kukarabati bwawa la Inga katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Josephat Nyiro Charo11 Agosti 2010

Mkuu wa benki ya Maendeleo ya Ujerumani kuipa Kongo msaada wa fedha kufanikisha ukarabati wa bwawa la Inga kwa uzalishaji wa umeme

https://p.dw.com/p/OidD
Bwawa la Inga nchini KongoPicha: AP

Ujerumani imesema inataka kulikarabati bwawa la umeme la INGA lilipo katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo pamoja na kujihusisha na huduma ya maji safi kwa wananchi wa Kongo. Kauli hiyo imetolewa na kiongozi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani, Doris Kohn ambaye yuko ziarani mjini Kinshasa. Kwa mara ya kwanza kabisa Ujerumani inatakiwa kuwekeza kiwango kikubwa cha fedha nchini Kongo licha ya kuweko na benki ya mikopo kwa ajili ya viwanda vidodo vidogo mjini Kinshasa. Taarifa kamili na mwandishi wetu wa Kinshasa, Saleh Mwanamilongo:

Mtayarishaji: Saleh Mwanamilongo

Mpitiaji: Grace Patricia Kabogo

Mhariri:Josephat Charo