1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kupeleka vikosi vya mapigano Afghanistan

7 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D3gG

BERLIN:

Ujerumani kwa mara ya kwanza imekubali kuchangia kikosi cha mapigano nchini Afghanistan kama sehemu ya vikosi vya Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi-NATO.Kikosi hicho cha wanajeshi 250 kitachukua nafasi ya kikosi cha Norway kitakapomaliza muda wake na kuondoka kaskazini ya Afghanistan baadae mwaka huu.Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Franz-Josef Jung amesema uamuzi huo umepitishwa kufuatia ombi la NATO.

Lakini Jung amesisitiza kuwa wanajeshi wa Ujerumani hawatopelekwa kusini mwa Afghanistan,ambako washirika wa NATO kama Uingereza,Kanada na Marekani wanapambana na uasi wa Wataliban.Kanada na Marekani zimetoa wito kwa wanachama wengine wa NATO kupeleka vikosi zaidi kusini mwa nchi.Hivi sasa, Ujerumani ina zaidi ya wanajeshi 3,000 kaskazini mwa Afghanistan kama sehemu ya kikosi cha kimataifa kusaidia kulinda usalama,chini ya uongozi wa NATO.