1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kuwasaidia wakimbizi wa Kipalestina

P.Martin2 Novemba 2007

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier amesema,Iran huenda ikawekewa vikwazo na Umoja wa Ulaya iwapo nchi hiyo haitoshirikiana kikamilifu na Shirika la Nishati ya Nyuklia la Umoja wa Mataifa-IAEA.

https://p.dw.com/p/C7fg

Waziri Steinmeier aliwaambia waandishi wa habari mjini Tel Aviv,Iran ina muda hadi katikati ya mwezi ujao kulithibitishia shirika hilo la kimataifa kuwa haijaribu kutengeneza silaha za kinyuklia.Steinmeier alitamka hayo baada ya mkutano wake pamoja na waziri wa nje wa Israel,Tzipi Livni.

Steinmeier vile vile amekutana na maafisa wa Kipalestina mjini Ramallah katika Ukingo wa Magharibi.Kwenye mkutano pamoja na waandishi wa habari mjini Ramallah,Steinmeier alitangaza kuwa Ujerumani itatoa msaada wa Euro milioni moja kwa ajili ya wakimbizi wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza-eneo linalodhibitiwa na Hamas. Msaada huo utatolewa kwa shirika la misaada la Umoja wa Mataifa linalotoa misaada kwa wakimbizi.