1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani na Ufaransa zapendekeza mabadiliko ya mkataba wa EU

6 Desemba 2011

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na Na Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa jana wamekubaliana mabadiliko kadhaa yenye lengo la kuinusuru sarafu ya euro na utekelezaji wa nidhamu ya matumizi miongoni mwa wanachama wa EU.

https://p.dw.com/p/13NHF
French President Nicolas Sarkozy, left, smiles as he greets German Chancellor Angela Merkel prior to their meeting at the Elysee Palace in Paris, Monday Dec. 5, 2011. The leaders of Germany and France will try to agree Monday on a cohesive plan to help save the euro through stricter oversight of government budgets. Financial markets signaled optimism that French President Nicolas Sarkozy and German Chancellor Angela Merkel will unveil a unified plan that tightens political and economic cooperation among the 17 European Union countries that use the euro and sets the stage for more aggressive aid from the European Central Bank. (Foto:Remy de la Mauviniere/AP/dapd)
Kansela Merkel na Rais SarkozyPicha: dapd

Viongozi hao wawili wamependekeza mabadiliko mapya katika mkataba wa ulaya, kwa lengo la kufanikisha lile linalokusudiwa mwishoni mwa Machi. Viongozi hao wamesema watawasilisha mipango yao kwa rais wa Umoja wa Ulaya Herman Van Rompuy hapo kesho ikiwa siku moja kabla ya mkutano mkubwa wa viongozi wote wa nchi 27 za Umoja wa Ulaya unatoarajiwa kufanyika Brussels keshokutwa.

Akizungumza katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mjini Paris baada ya mkutano wao wa muda mrefu, Merkel amesema wana nia ya uhakika kuiletea utulivu sarafu ya euro na kuimirisha ushindani katika kanda ya euro.

Pamoja na mambo mengine mkataba huo mpya utajumuisha vikwazo vya moja kwa moja kwa wanachama watakaokiuka kanuni.Kimsingi mkataba huo utaidhinishwa na nchi zote 27 za Umoja wa Ulaya lakini Sarkozy alisema saini za nchini 17 zinazotumia sarafu ya euro zitakubaliwa.