1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani na Uturuki leo

25 Juni 2008

Leo ni nusu-finali ya kombe la Ulaya baina ya Ujerumani na Uturuki.

https://p.dw.com/p/EQa5
Ballack na wenzake.Picha: AP

Leo ni nusu -finali ya kwanza ya kombe la Ulaya kati ya Ujerumani na Uturuki,mjini Basel, Uswisi.Changamoto hii ikisubiriwa kwa hamu kuu kati ya mashabiki wa timu hizo mbili na nchini Uturuki na Ujerumani,kwavile wanaishi humu nchini si chini ya waturuki milioni 2.5.Bendera za Ujerumani na za Uturuki zinapepea juu ya motokaa na majumba .

Party zimeandaliwa usiku wa leo katika miji na mitaa mbali mbali ya Ujerumani na hasa mjini Berlin ambako hadi waturuki laki moja wanaishi.

►◄

Ujerumani yatazamiwa leo kutamba mbele ya Uturuki na jumapili hii kutwaa taji lake la 4 la kombe la Ulaya.

Timu ya kocha Joachim Loew,iliopigiwa upatu kabla kuanza kombe hili la Ulaya, ingelitwa ubingwa ,ilichukua muda kabla haikuanza kutamba na hata ilishindwa mara 1 na Croatia.Lakini baada ya kuitimua Ureno kwa mabao 3-2,imani ilirejea kwa mashabiki na mahasimu wa Ujerumani kuwa ndio timu itakayotamba.

Kumbuka Ujerumani imetawazwa mabingwa wa Ulaya na dunia mara 3 na imeibuka makamo-bingwa si chini ya mara 6 tangu ilipojitosa katika mashindano ya kombe la dunia, 1934 nchini Itali.

Hatahivyo, Uturuki huwezi kuitoa maanani na kudai itakua bonde tu la kuteremka.Uturuki hadi sasa imeonesha uvumilivu mkubwa wa kuhimili vishindo vya kombe la ulaya na ukaidi usio na kifani wa kutokubali kukata roho na mapema.Imeshinda mechi zake ikitia mabao 3 mnamo robo-saa ya mwisho.

Lakini, kikosi hiki cha kocha Fatih Terim kimetetereka mguu ,kwani hadi wachezaji 6 ni hoi.Matumaini kwamba nahodha wao Emre Belozoglu, atarudi uwanjani baada ya kuumia katika ile mechi ya kwanza dhidi ya Ureno, jana hayakutimilia.

Ujerumani kinyume na Uturuki,haina tena walioumia.Mchezaji wao kiboko wa kiungo kwa mashambulio Torston Frings amepona .Kuumia kwa Frings kuliongoza Ujerumani kubadili mchezo wake kutoka staili ya 4-4-2 anayoipendelea kocha Loew na kugeukia 4-5-1 iliovunja ubishi wa wareno.sasa Loew anaumwa na kichwa hajui atumie leo mfumo gani kati ya hiyo 2.

Nahodha wa Ujerumani ameshika barabara usukani wa jahazi lake.Michael Ballack anasema Ujerumani itayari na wamejiandaa barabara kwa zahama za leo usiku.

I"Yaliokua mapumziko marefu kutoka mechi moja kwenda nyengine.Timui yetu ina hamu sana ya kucheza dimba.Tumekua na mazowezi 2 na nadhani tumejiandaa barabara."

Nani atashinda leo na kutoroka mwishoe na kombe la Ulaya pengine ni vigumu kuagua-kwani maajabu mengi yamezuka katika kom,be hili:wa wapi mabingwa na makamo-bingwa wa dunia-Itali na Ufaransa.Na wawapi Holland waliotamba.

Kocha wa Arsenal London,Arsene Wenger anadai ujerumani itatawazwa mabingwa wa Ulaya 2008 na ndio itakayocheza finali ya jumapili kati yake na Spian,mjini Vienna. Wenger amesema Ujerumani ina tabia ya kumudu vishindo vyote na yenye kujiaamini-sifa ambayo timu nyengine hazina.Waturuki wangembisha Wenger au ?