1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yachunguza madai ya kupewa sumu mwandishi habari

Sudi Mnette
21 Mei 2023

Gazeti la kila Jumapili la hapa Ujerumani- Welt am Sonntag limeripoti kuwa polisi wa Ujerumani wameanzisha uchunguzi baada ya mwandishi wa habari wa Urusi na mwanaharakati kudaiwa kupewa sumu.

https://p.dw.com/p/4Rd60
Standbild DW Interview Michail Chodorkowski
Picha: DW

Gazeti la kila Jumapili la hapa Ujerumani- Welt am Sonntag limeripoti kuwa polisi wa Ujerumani wameanzisha uchunguzi baada ya mwandishi wa habari wa Urusi na mwanaharakati walioshiriki katika mkutano wa Berlin kupatwa na matatizo ya kiafya yaliyodhaniwa kuwa yametokana na uwezekano wa kuwekewa sumu.Licha ya Shirika la Habari la Ufaransa AFP, kushindwa kupata kauli ya polisi kuhusiana na hatua hiyo lakini gazeti hilo limeandika kuwa jalada limefunguliwa  kwa zingatio la taarifa za wazi. Chombo cha habari za uchunguzi cha Urusi "Agentstvo" katika uchuguzi wake wa juma hili kiliripoti juu ya matatizo ya kiafya waliokabiliano nayo washiriki wawili katika mkutano wa wapinzani wa Urusi wa Aprili 29 na 30 ulioratibiwa na tajiri wa zamani wa Urusi anayeishi uhamishoni ambaye ni mkosoaji mkubwa wa serikali ya Kremlin, Mikhail Khodorkovsky.