1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yadai serikali ya taifa Kenya

5 Januari 2008

---

https://p.dw.com/p/Cklw

Nae waziri wa misaada ya maendeleo wa Ujerumani Bibi Heidemarie Wieczoreck-Zeul amejiunga na mwito uliotolewa tangu kwa serikali ya Kenya hata kwa vyama vya upinzani kutatua ugomvi wao kwa mazungumzo.Katika taarifa yake, waziri huyo wa Ujerumani alisema anaungamkono pendekezo alilotoa waziri-mkuu wa Uingereza Gordon Brown kwamba pande mbili zinazogombana nchini Kenya zijaribu kuunda serikali ya umoja wa Taifa.

Wizara ya nje ya Ujerumani imetangaza huko Berlin kwamba inapeleka msaada wa Euro laki 3 kupitia chama cha msalaba mwekundu ulimwenguni kuwasaidia wakenya waliopoteza maskani zao kutokana na machafuko ya sasa ya uchaguzi.