1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yailaza Uholanzi 2-1

Josephat Nyiro Charo14 Juni 2012

Katika fainali za kugombea kombe la mataifa ya Ulaya, Uefa Euro 2012, Ujerumani imeshajiweka katika njia iliyonyooka ya kueleka katika robo fainali.

https://p.dw.com/p/15EQR
Germany's players celebrate their victory at the end of their Group B Euro 2012 soccer match against Netherlands at the Metalist stadium in Kharkiv, June 13, 2012. REUTERS/Michael Buholzer (UKRAINE - Tags: SPORT SOCCER)
Timu ya Ujerumani ikisherehekea ushindiPicha: Reuters

Timu ya Ujerumani iliutekeleza wajibu wake barabara uwanjani kwa kuichapa Uholanzi mabao mawili kwa moja. Mabao hao yote yalifungwa na Mario Gomez na hivyo kuiweka Ujerumani katika nafasi ya kwanza ya kundi B.

Lakini kabla ya mechi kuanza Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle, alitoa mwito kwa wapenzi wote wa kandanda kutomsahau kiongozi wa upinzani nchini Ukraine Yulia Tymoshenko Tymoshenko aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ukraine ambako mashindano ya kugombea kombe la mataifa ya Ulaya yanafanyika, anatumikia kifungo cha miaka saba jela kwa kosa la kuyatumia vibaya madaraka alipokuwa waziri Mkuu. Wanaomuunga mkono mwanasiasa huyo wanasema kuwa adhabu aliyopewa imetokana na sababu za kisiasa.

Gomez ang'ara

Tukirejea uwanjani katika mji wa Kharkiv nchini Ukraine, Mshambuliaji wa Ujerumani Mario Gomez aliingozea timu yake pointi 3 kutokana na magoli yake mawili hapo jana na kuwapa Wajerumani matumaini makubwa zaidi safari hii ya kurudi nyumbani na kombe. Kutokana na ushindi wa jana Ujerumani sasa inaongoza katika kundi B ikiwa na ponti sita wakati timu za Denmark na Ureno zina ponti tatu kila mmoja katika kundi hilo. Waholanzi ambao ni makamu bingwa wa kandanda duniani, sasa wanashika mkia katika kundi hilo.

Germany's Mario Gomez, right, scores the opening goal past Dutch goalkeeper Maarten Stekelenburg, left, during the Euro 2012 soccer championship Group B match between the Netherlands and Germany in Kharkiv, Ukraine, Wednesday, June 13, 2012. (Foto:Vadim Ghirda/AP/dapd)
Mario Gomez akifunga bao la kwanzaPicha: AP

Kilio cha kwanza cha Waholanzi kilikuja katika dakika ya 24 ambapo Gomez alimlazimisha kipa wa uholanzi kuangilia nyuma ya goli lake na kuona jinsi wavu ulivyokuwa unatingisika. Dakika ya 38 mambo yalijirudia kwenye uwanja wa mjini Kharkiv. Timu ya Ujerumani iliongoza kwa mabao mawili. Lakini nani asiyewajua Waholanzi kwa ujasiri wao.

Walipigana kufa na kupona hadi juhudi zao zilipozaa matunda. Katika dakika ya 73 mshambuliaji maarufu Robin van Persie aliutikisa wavu wa goli la timu ya Ujerumani. Lakini bao hilo halikutosha kuwaondoa waholanzi katika hatari ya kurudi nyumbani mapema.

Netherlands' Robin van Persie celebrates after scoring a goal during their Group B Euro 2012 soccer match against Germany at the Metalist stadium in Kharkiv, June 13, 2012. REUTERS/Michael Buholzer (UKRAINE - Tags: SPORT SOCCER)
Robin van Persie ashangiliaPicha: Reuters

Ureno yaichapa Denmark

Katika mechi nyingine ya kundi B Wareno walifanikiwa kuyarudisha matumaini ya kuendelea kuwamo katika kinyang'anyiro cha kugombea kombe la mataifa ya Ulaya. Timu ya Ureno ilicheza kwa ustadi mkubwa kwenye uwanja wa Arena Lviv katika mji wa Lviv nchini Ukraine na kuichapa timu ya Denmark mabao matatu kwa mawili. Hata hivyo ushindi wa timu ya Ureno ulipatikana baada ya wachezaji wa timu hiyo kupania kweli kweli. Pumzi ya faraja ilikuja katika dakika ya 24 ambapo beki Pepe aliliona lango la Denmark kwa goli la kichwa.

Portugal's Pepe celebrates scoring a goal against Denmark during their Group B Euro 2012 soccer match at the New Lviv stadium in Lviv June 13, 2012. REUTERS/Michael Dalder (UKRAINE - Tags: SPORT SOCCER)
Pepe akifurahia bao lakePicha: Reuters

Furaha ya Wareno iliongezeka katika dakika ya 36, baada ya Helder Postiga kufunga goli la pili. Lakini wasiwasi ulirudi kwa wareno baada ya Denmark kuyarudisha magoli hayo mawili. Mpaka alipopatikana shujaa wa mechi kutokea kwenye kivuli cha benchi. Jina lake ni Silvestre Varela. Na ndiye aliyewaletea Wareno ushindi kwa bao lake ambalo lilikuwa la tatu kwa Wareno. Katika hatua inayofuata katika kundi B Ujerumani itapambana na Denmark na Uholanzi itamenyana na Ureno.

Mwandishi:Mtullya Abdu/dpae/ZA/afp/rts

Mhariri: Josephat Charo