1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaisambaratisha Uingereza

29 Juni 2010

Ujerumani imeichabanga Uingereza mabao 4-1 na kuingia robofainali ya kombe la dunia kwa kishindo kikubwa.

https://p.dw.com/p/O4Vc
Wachezaji wa Ujerumani wakishangilia ushindiPicha: AP

Uingereza ilikataliwa bao lake la kusawazisha, la mkwaju wa Frank Lampard, lakini hata hivyo ilishindwa kabisa kuzuia kasi ya wachezaji wa Ujerumani.

Flash-Galerie Fußball WM 2010 Südafrika Achtelfinale Deutschland vs England
Mlinda mlango wa Ujerumani Manuel Neuer akiangalia mpira uliyopigwa na Lampard ukivuka msmatari wa goli kbal ya kuudaka.Picha: AP

Mabao ya Ujerumani yaliwekwa wavuni na Mirosla Klose, Lukas Podoski na Thomas Muller aliyepachika mawili.

Katika mechi hiyo iliyokuwa akisubiriwa kwa hamu kubwa kote duniani, mshambuliaji wa Bayern Munich Thomas Muller alichaguliwa kuwa mwanasoka bora wa mechi.

Ujerumani sasa itapambana na mshindi kati ya Argentina na Mexico.

Mwandishi:Aboubakary Liongo