1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yajivunia ukuaji madhubuti wa kiuchumi

Oummilkheir5 Julai 2007

Waziri wa uchumi Michael Glos achekelea ukuaji wa kiuchumi utapindukia asili mia mbili nukta tatu

https://p.dw.com/p/CHBZ
Wazirfi wa uchumi (kulia mwa kansela Merkel)
Wazirfi wa uchumi (kulia mwa kansela Merkel)Picha: AP

Waziri wa uchumi wa serikali kuu ya Ujerumani Michael Glos anaendelea kuamini ukuaji wa kiuchumi kwa mwaka huu utafikia asili mia 2.3.Suala wadadisi wanalojiuliza ni jee kipi cha kufanywa ili kuzidi kuimarisha ukuaji wa kiuchumi?Waziri wa uchumi Michael Glos amefafanua zaidi katika hotuba yake mbele ya bunge la shirikisho Bundestag mjini Berlin.

Watu milioni 40 wanafanya kazi nchini Ujerumani-idadi kubwa kama hiyo haijawahi kushuhudiwa hapo awali.Zaidi ya hayo idadi ya wasiokua na ajira inapungua.Na mwakani uchumi unatarajiwa kuzidi kukua.Tarakimu hizo zinamfanya atabasamu na kuridhika waziri wa uchumi wa serikali kuu Michael Glos .Ujerumani inashika tena usukani wa ukuaji wa kiuchumi barani Ulaya-anesema waziri huyo wa uchumi wa kutoka chama cha Christian Social Union CSU.Shukurani ziiendee serikali ya shirikisho.

“Sasa hasa ndio tunabidi kuendelea na mkondo wa mageuzi.Mkakati wa ncha tatu wa serikali ya muungano wa kusawazisha,kurekebisha na kuwekeza,unazaa matunda hivi sasa.“

Lakini matokeo hayo ya kutia moyo hayastahiki kuwafanya wanasiasa wasijiachie tuu-miche iliyozaa matunda hayo inabidi itunzwe na kupaliliwa.Waziri wa uchumi Michael Glos anapigania haja ya kuendelea kuimarishwa bajeti.Zaidi ya hayo anahisi waziri Glos raia wahusishwe pia na ukuaji wa kiuchumi mfano kwa kupunguziwa michango ya bima ya uzeeni.

Wasi wasi wa waziri wa uchumi wa serikali kuu ya Ujerumani unakutikana hasa katika tatizo linalosababishwa na uhaba wa wajuzi.Kwa wakati huu tulionao makampuni ya Ujerumani yana ukosefu wa wahanadisi 40 elfu.

Waziri wa uchumi Michael Glos anaendelea kusema:

„Ndio maana tunabidi tuendelee kuwekeza katika sekta ya elimu na mafunzo ya kazi.Tunabidi kwanza tuwapatie watu mafunzo ya kazi na kuwapa amoyo wasalie hapa nchini.Hapo linazuka pia suala la kuwapata wasomi wa kutoka ng’ambo ambalo tutabidi tulishughulikie mapema na kurahisisha mambo “

Waliberali pia wanahimiza suala hilo lishughulikiwe.Kwa maoni yao mageuzi ya kiuchumi ya serikali kuu ya muungano hayendi mbali sana.“Wakati umewadia sasa wa kupunguza kodi za mapato na kuregeza kamba katika sheria za soko la ajira“ anasema kwa mfano Rainer Brüderle wa kutoka chama cha upinzani cha FDP.

Lawama kali zaidi zimetolewea na mrengo wa shoto.Greogor Gysi anaikosoa serikali kuu akihoji ukuaji wa kiuchumi unawanufaisha sehemu ndogo tuu ya wananchi.Anapendekeza fedha ziada zilizoingia toka malipo ya kodi uzitumiwe kugharimia bima za jamii ikiwa ni pamoja,bima ya uzeeni,bima ya afya na bima ya wasiokua na ajira.

Walinzi wa mazingira wanakosoa ile hali ya kutokuwepo na mpango madhubuti wa kuimarisha ukuaji wa kiuchumi.

Vyama vinavyounda serikali kuu ya muungano mjini Berlin havishughulishwi lakini na lawama hizo.Kuna kinachowashughulisha zaidi nacho ni mvutano kuhusu nani hasa chanzo cha ukuaji huu wa kiuchumi : CDU,CSU au SPD?