1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yasema itaiunga mkono Ugiriki

Sekione Kitojo16 Januari 2012

Ujerumani imeihakikishia Ugiriki kuwa itafanya kila inaloweza kuiunga mkono na kuikingia kifua katika matatizo yake ya madeni.

https://p.dw.com/p/13k8j
Bundesaussenminister Guido WESTERWELLE, FDP, Portraet, Portrait, Begruessung der Delegationen, World Conference Center Bonn, 4. Internationale Afghanistan-Konferenz in Bonn, 05.12.2011,
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido WesterwellePicha: picture-alliance/dpa

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle ameihakikishia serikali ya Ugiriki kuwa Ujerumani itasimama pamoja na Ugiriki. Katika ziara yake nchini Ugiriki , alikutana na waziri mkuu wa nchi hiyo Lucas Papademos pamoja na waziri wa mambo ya kigeni Stavros Dimas.

Greek Prime Minister Lucas Papademos delivers a speech at Greek Parliament in Athens, Monday, Nov. 14, 2011. Greece's junior coalition leader Conservative party leader Antonis Samaras defied European demands to provide written support for a massive new debt relief deal, leaving the country's loan lifeline in doubt hours before its new government was to outline its policy platform. (Foto:Thanassis Stavrakis/AP/dapd)
Waziri mkuu wa Ugiriki Lucas PapademosPicha: dapd

Westerwelle ameweka wazi kuwa Ugiriki ina nafasi katika bara la Ulaya. Westerwelle pia amesema kuwa huu ndio wakati ambao bara la Ulaya linapaswa kushughulikia hatua ya mashirika ya kuweka viwango vya ukopaji na kutuliza masoko.

Akizungumza kwa lugha ya kiingereza kusisitiza suala hilo, ametilia mkazo kuwa makubaliano na mikataba iliyofikiwa na mataifa wanachama wa umoja wa Ulaya inahitaji kupewa nafasi ili kufanyakazi.

Siku ya Ijumaa , shirika la Standard and Poors lilishusha viwango vya mataifa tisa ya Ulaya , miongoni mwao ikiwa ni Ufaransa, ambayo imepoteza alama yake ya juu ya A tatu.