1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yawakumbuka wahanga wa mauaji ya kuangamiza

Mohammed Khelef
27 Januari 2023

Ujerumani leo inawakumbuka wahanga wa utawala wa Kinazi waliouawa kwenye mauaji ya maangamizi kuelekea mwishoni mwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

https://p.dw.com/p/4Mmap
Berlin | Der Deutsche Bundestag gedenkt der Opfer des Holocaust in Berlin
Picha: Michele Tantussi/REUTERS

Miongoni mwao ni aliyenusurika na mauaji ya Wayahudi, Rozette Kats, ambaye atazungumza katika kumbukumbu hiyo inayofanyika kwenye Bunge la Ujerumani.

Spika wa Bunge la Ujerumani, Bärbel Bas atafungua tukio hilo muhimu, ambalo pia linahudhuriwa na Rais wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier.

Soma zaidi: Siku ya kimataifa ya kumbukumbu ya mauaji ya Holocaust ni nini?

Kumbukumbu ya mwaka huu inawaangazia watu ambao waliteswa na utawala wa Wanazi kwa sababu ya mwelekeo wao wa kijinsia au utambulisho wao.

Januari 27 mwaka 1945, wanajeshi wa Urusi waliwakomboa watu walionusurika na mauaji katika kambi ya mateso na maangamizi dhidi ya Wayahudi ya Auschwitz nchini Poland.

Utawala wa Wanazi uliwaua zaidi ya watu milioni moja, wengi wao wakiwa Wayahudi.