1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe mkali kwa Mugabe

20 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CJVf

Umoja wa Ulaya hapo jana umekubali kutowa ujumbe wa wazi na mkali kwa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe juu ya haki za binaadamu wakati wa mkutano wa kilele na viongozi wa Afrika mwezi ujao pamoja na kumtuma mjumbe nchini humo kabla ya mkutano huo.

Mkutano huo uliopangwa kufanyika tarehe nane na tisa mwezi wa Desemba nchini Ureno utakuwa wa kwanza kufanyika kati ya mabara hayo mawili katika kipindi cha miaka saba.Juhudi za kufanyika kwa mkutano huo huko nyuma zimekuwa zikikwamishwa kutokana na suala la kualikwa kwa Mugabe ambaye mataifa ya magharibi yanamshutumu kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu.

Ukikabiliwa na ushindani wa biashara wa China kwa Afrika Umoja wa Ulaya unataka mkutano huo ufanyike na safari hii imemualika Mugabe licha ya tishio la Uingereza kuususia mkutano huo.