1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Mawaziri wa Korea Kaskazini kuanza ziara nchini Iran

24 Aprili 2024

Ujumbe wa viongozi kutoka Korea Kaskazini ukiongozwa na Waziri wa biashara wameelekea nchini Iran katika ziara ya nadra baina ya viongozi wa mataifa hayo mawili.

https://p.dw.com/p/4f75D
Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un
Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong UnPicha: KCNA/AP Photo/picture alliance

Mataifa hayo yamekuwa yakishukiwa kuwa na mahusiano ya siri ya kijeshi. Taarifa hiyo imetolea na shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini KCNA.

Waziri anayehusika na mahusiano ya kiuchumi wa Korea Kaskazini Yun Jong Ho, ameondoka jana mjini Pyongyang kuelekea Iran akiongozana na mawaziri wengine kadhaa. Hata hivyo vyombo vya habari nchini humo havikutoa taarifa zaidi.

Korea Kaskazini na Iran kwa muda mrefu zimekuwa zikishukiwa kushirikiana kwenye programu za makombora ya masafa marefu, na pia kubadilishana utaalamu wa kiufundi na hata vifaa vinavyotumiwa katika  utengenezaji wa silaha hizo.

Mataifa hayo mawili yamekuwa yakishutumiwa pia kuisaidia Urusi katika uvamizi wake nchini Ukraine kwa kuipatia makombora na silaha zingine.