1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe wa umoja wa nchji za kiarabu waelekea Israel

Mohammed Abdul-Rahman25 Julai 2007

Ni ziara ya kwanza kuwahi kufanywa na umoja huo, huku jitihada za kusaka amani ya mashariki ya kati zikipata kasi.

https://p.dw.com/p/CHAX
Mfalme Abdullah II ambaye naye yuko washington.
Mfalme Abdullah II ambaye naye yuko washington.Picha: AP

Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Jordan na Misri wanatarajiwa kuwasili Israel leo kwa mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo, katika jitihada za kuupa msukumo mpango wa amani ulioidhinishwa na umoja wa nchi za kiarabu.

Kwa upande mwengine Mfalme Abdullah wa pili wa Jordan amekua na mazungumzo na rais wa Marekani George W. Bush mjini Washington.

Mawaziri hao wa mambo ya nchi za nje wa Jordan na Misri Abdel Ilah al-khatib na Ahmed Abul Gheith, watakuweko Jerusalem kwa siku nzima wakiwa na mlolongo wa mazungumzo na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert, waziri wa mambo ya nchi za nje Tzipi Livni na Waziri wa ulinzi Ehud Barak pamoja na wabunge.

Halikadhalika wanatarajiwa kukutana na kiongozi wa chama cha upinzani cha mrengo wa kulia Benjamin Netanyahu na rais wa Israel Shimon Peres.

Misri na Jordan nchi pekee za kiarabu zilizotiliana saini mkataba wa amani na Israel zinatarajia kuishawishi dola ya kiyahudi iukubali mpango wa amani wan chi za kiarabu, ambao ulipitiwa upya karibnuni na Saudi aarabia na kuidhinishwa tena na umoja wa nchi za kiarabu.

Umoja huo wa wanacahama 22 umezipa jukumu Misri na Jordan kuishawishi Israel iukubali mpango huo wa amani uliopitishwa mjini Riyadh na viongozi wa kiarabu mwezi Machi .

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Jordan Khatib alisema watawasilisha ujumbe kwa Israel kwamba juhudi za dhati za pamoja kuelekea amani zitakua ni tija kwa eneo hilo.

Kwa mujibu wa mpango huo, nchi za kiarabu zitakua tayari kurejesha uhusiano na Israel na badala yake Israel iondoke katika ardhi za waarabu ilizoziteka katika vita vya siku 6 vya 1967, kuundwa dola ya palestina na kurudi nyumbani wakimbizi wakipalestina.

Israel ambayo iliupinga mpango huo ulipozinduliwa hapo awali wakati wa mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi za kiarabu mjini Beirut 2002, imesema tangu wakati huo kwamba unaweza kuwa msingi wa mazungumzo pindi ukifanyiwa marekebisho kuhusiana na suala la wakimbizi wakipalestina.

Ziara hii ya ujumbe wa umoja wa nchi za kiarabu mjini Jerusalem ya kwanza kufanywa na umoja huo nchini Israel, imekuja katika wakati ambao Mfalme Abdullah wa pili wa Jordan yuko Washington na katika mazungumzo yake na Rais George W. Bush alimshinikiza kiongozi huyo wa Marekani iimarishe jitihada za kusaka amani ya Masahariki ya kati, na kwamba Israel haina budi kuondoa vizuizi kwa nyendo za wapalestina.

Mfalme huyo alisema kwamba amani ya haki nay a kudumu ambayo umma wa kiarbu unaipigania, lazima itokane na suluhisho litakalozingatia na kuyatatua masuala yote ya msingi baina ya wapalestina na Israel .

Kwa upande wake rais Bush alielezea juu ya kujizatiti kwa nchi ayake katika kuunga mkono juhudi za kusaka amani katika eneo hilo chini ya msingi wa dola mbili Israel na Palestina. Aidha viongozi hao wawili walizungumzia pia suala la Irak.

Wakati huo huo mjumbe wa pande nne zinazohusika na amani ya mashariki ya kati, Umoja wa mataifa, Umoja wa ulaya, Marekani na Urusi, waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair, amemaliza mazungumzo na Waziri mkuu wa Israel Olmert na rais wa Palestina Mahmoud Abbas. Bw Olmert amesisitiza kwa mara nyengine kwamba nchi yake haitokubali kushirikishwa chama cha Hamas katika mazungumzo na akataka kiendelee kutengwa.

Baadae akizungumzia kutegwa kwao msemaji wa Hamas , Ghazi Hamad alisema Tony Blair si waziri mkuu tena wa Uingereza bali ni mjumbe anayetafuta amani, hivyo hana budi kuzungumza na kuzisikiliza pande zote zinazohusika.